Umoja wa Mataifa: Sudan inakabiliwa na janga kubwa la njaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i136344-umoja_wa_mataifa_sudan_inakabiliwa_na_janga_kubwa_la_njaa
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, nchi ya Sudan inayoshuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe inakabiliwa na njaa kali.
(last modified 2026-02-07T02:46:06+00:00 )
Feb 07, 2026 02:46 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Sudan inakabiliwa na janga kubwa la njaa

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, nchi ya Sudan inayoshuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe inakabiliwa na njaa kali.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa, watoto katika maeneo ya jimbo la Darfur ya kaskazini nchini Sudan wanakabiliwa na utapiamlo kiwango cha kuweza kuleta maafa, kutokana na mapigano yanayoendelea na kusababisha watu wengi kuhama makaazi yao kutokana pia na ukosefu wa upatikanaji misaada.

Shirika la Usalama wa Chakula Duniani (WFP) linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa limesema kuwa, maeneo ya Um Baru na Kernoi yako katika hali mbaya zaidi kwa njaa, kufuatia kushambuliwa mji mkuu wa eneo hilo El Fasher Oktoba mwaka 2025 ambapo idadi kubwa ya watu walikimbilia usalama wao.

Tathmini iliyofanywa mwezi Desemba inaonyesha kwamba, kiwango cha utapiamlo kwa watoto katika eneo la Um Baru ni asilimia 52.9 ikiwa ni ongezeko la mara mbili zaidi na katika eneo la WFP imetahadharisha kuwa, viwango vya utapiamlo vinatarajiwa kuongezeka zaidi huku zaidi ya watoto na wanawake milioni nne kote nchini Sudan wakitarajiwa kuathiriwa mwaka huu katika wakati ambao vita vya wenyewe kwa wenyewe vingali vinaendelea.

Vita nchini Sudan, vilivyoanza Aprili 2023 kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa RSF, vimeharibu mifumo ya chakula nchi nzima, na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao, masoko kusambaratika pamoja na adha ya kupata huduma za afya, maji na lishe. Hayo yanajiri katika hali ambayo, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo wa Sudan hadi sasa hazijazaa matunda.