-
Baraza la Haki za Binadamu la UN linapigia kura rasimu ya azimio kuhusu Sudan
Nov 14, 2025 05:41Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa, litapiga kura katika kikao maalumu kinachojadili mgogoro wa Sudan, kuhusu rasimu ya azimio linalolaani ukiukwaji wa haki za binadamu ambao linasema umefanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ndani na karibu na mji wa El Fasher katika shambulio la hivi karibuni la wapiganaji wa kundi hilo dhidi ya mjini huo.
-
Kwa nini kutoshiriki Marekani katika kikao cha G20 nchini Afrika Kusini ni hasara kubwa kwa Washington?
Nov 14, 2025 04:39Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa kutohudhuria Wamarekani katika kikao cha G20 ni hasara kubwa kwao.
-
UN yamchagua Profesa Phoebe Okowa wa Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya ICJ
Nov 14, 2025 04:12Katika kura ya kihistoria iliyopigwa Umoja wa Mataifa siku ya Alkhamisi, profesa wa sheria wa Kenya Phoebe Okowa alichaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), akiibuka mshindi kwenye ulingo wa ushindani wa wagombea wa Kiafrika baada ya mfululizo wa raundi za kupiga kura zilizokuwa na mvutano katika Baraza Kuu na Baraza la Usalama.
-
Bunge la Tanzania lamthibitisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo
Nov 13, 2025 10:20Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Alhamisi limemthibitisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo baada ya kupata kura 369 kati ya kura 371 zilizopigwa na wabunge. Baada ya uthibitisho huo, Dkt. Nchemba ataapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuanza mara moja majukumu yake.
-
Mudavadi: Zaidi ya Wakenya 200 wanapigana pamoja na Russia katika vita vya Ukraine
Nov 13, 2025 10:19Serikali ya Kenya imesema kwamba zaidi ya raia wake 200 wanapigana katika safu ya jeshi la Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, ikionya kwamba mitandao ya kuajiri wapiganaji bado inaendelea kufanya kazi na inawalenga Wakenya kwa kutoa kazi zenye kipato kikubwa.
-
Ni ipi nafasi ya pande za kigeni katika mgogoro wa Sudan?
Nov 13, 2025 09:25Vita nchini Sudan vimechukua sura mpya kufuatia kuendelea uingiliaji kati wa nchi ajinabi nchini humo na kudhibitiwa mji wa Al Fasher na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Katibu Mkuu wa UN: Dunia isiliache mkono bara la Afrika, lina uwezo mkubwa mno
Nov 13, 2025 09:05Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema dunia haiwezi kulipa kisogo bara la Afrika akisisitiza kuwa bara hilo ni nyumbani kwa karibu robo ya watu wote duniani, na lina nafasi kubwa ya maendeleo.
-
Mali yakanusha hofu kwamba magaidi wanakaribia kuudhibiti mji mkuu, Bamako
Nov 13, 2025 09:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali amepuuzilia mbali dhana kwamba magaidi hivi karibuni wanaweza kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako. Hii ni radiamali ya kwanza kutolewa na serikali kuhusu wasiwasi na hofu ya usalama katika nchi ya Mali ambayo imechochea nchi za Magharibi kuwataka raia wao waondoke nchini humo.
-
Kamisheni ya Umoja wa Afrika yakanusha madai ya Trump kuhusu mauaji ya Wakristo Nigeria
Nov 13, 2025 03:50Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) amekanusha vikali madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mauaji ya kimbari dhidi ya Wakristo kaskazini mwa Nigeria.
-
Rais wa Afrika Kusini: Kutohudhuria Marekani mkutano wa G20 ni hasara kwake
Nov 13, 2025 03:48Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa, kitisho cha Rais wa Marekani Donald Trump kwamba maafisa wa nchi yake hawatahudhuria mkutano wa G20 mjini Johannesburg ni hasara kwa Wamarekani.