AU, ECOWAS zalaani jaribio la mapinduzi Benin; zasema zinaiunga mkono serikali
-
ECOWAS, AU
Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) zimelaani jaribio la mapinduzi nchini Benin siku ya Jumapili, na kueleza kuwa zinaiunga mkono serikali katika kudumisha utaratibu wa kikatiba.
Mahmoud Ali Youssouf Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amewataka waliopanga jaribio la mapinduzi kusitisha mara moja "vitendo vyote visivyo halali," kuheshimu Katiba ya Benin, na kurejea mara moja kwenye kambi zao na majukumu yao ya kitaaluma.
Youssouf ameeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuongezeka idadi ya mapinduzi ya kijeshi na majaribio ya mapinduzi barani Afrika na kukosoa vitendo hvyo kwamba vinadhoofisha vinadhoofisha uthabiti wa bara la Afrika na kutishia mafanikio ya kidemokrasia.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa mara nyingine tena ametilia mkazo "msimamo wa AU wa kutovumilia mabadiliko yoyote ya kikatiba ya serikali, bila kujali muktadha au uhalali wake."
Wakat huo huo Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imeahidi kuiunga mkono serikali ya Benin ili kuilinda katiba ya nchi hiyo na mamlaka ya kujitawala nchi hiyo.
ECOWAS imesema kuwa waliopangamapinduzi ya jana huko Benin wanabeba dhima kwa kwa maafa yoyote ya maisha na mali yaliyosaabishwa na hatua yao hiyo.
Kundi la wanajeshi wa Benin jana waliliambia shirika la utangazaji la nchi hiyo kwamba wamemuondoa madarakani Rais Patrice Talon madarakani na kumteua Luteni Kanali Pascal Tigri kuongoza “Kamati ya Kijeshi ya Uhuishaji Mpya waliyoiunda.
Muda mfupi baadaye, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Benin Alassane Seidou alisema kupitia teevisheni ya nchi hiyo kwamba wamezima jaribio la mapinduzi lililofanywa na kundi dogo la wanajeshi na kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.