-
IOM: Hatua za haraka zinahitajika ili kuwanusuru mamilioni ya raia walioathiriwa na vita Sudan
Nov 11, 2025 04:21Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) limetaka kuchukuliwa hatua za haraka ili kuwasaidia mamilioni ya raia walioathiriwa na vita vya Sudan kati ya jeshi la nchi hiyo na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Amnesty International yaitaka Nigeria kuwaondoa hatiani wanaharakati tisa waliouawa miaka 30 iliyopita
Nov 11, 2025 02:45Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeitaka serikali ya Nigeria kuwafutia kabisa hatia wanaharakati tisa wa mazingira waliouawa miaka 30 iliyopita, ambao walipigania kulinda eneo la Niger Delta kutokana na shughuli za kampuni kubwa ya mafuta ya Shell.
-
Mkurugenzi Mkuu wa WHO ataka kusitishwa umwagaji damu nchini Sudan
Nov 10, 2025 23:39Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametaka kusitishwa ghasia nchini Sudan baada ya kuuawa daktari katika mji ulioathiriwa na vita wa Al Fasher.
-
Kiongozi wa mapinduzi ya Guinea, Mamady Doumbouya aidhinishwa kuwania urais
Nov 10, 2025 23:35Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi wa Guinea Conakry, Mamady Doumbouya na wagombea wengine wanane wameidhinishwa kugombea katika uchaguzi wa rais mwezi ujao. Hii ni kwa mujibu wa orodha ya wagombea wa kiti cha urais iliyotolewa na Mahakama Kuu ya nchi hiyo.
-
Magaidi 200 wauawa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi nchini Nigeria
Nov 10, 2025 23:26Mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha vifo vya magaidi wasiopungua 200 katika eneo la Ziwa Chad.
-
Binti wa Zuma akana mashtaka ya uchochezi
Nov 10, 2025 23:22Duduzile Zuma-Sambudla, bintiye rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amekana mashtaka ya kuchochea ghasia wakati wa machafuko makubwa yaliyotokea nchini humo mwezi Julai 2021.
-
Hatari ya ushawishi wa Israel barani Afrika; Tishio lililofichika kwa uhuru wa bara Afrika
Nov 10, 2025 09:35Katika juhudi zake za kuitoa Israel kwenye hali ya kutengwa, Isaac Herzog, rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, anatarajiwa kuelekea barani Afrika.
-
Gavana wa Darfur: Al Burhan aamuru vikosi kusonga mbele kuelekea magharibi
Nov 10, 2025 08:43Gavana wa Darfur na kiongozi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan, Minni Arko Minnawi amesema kwamba mkuu wa Baraza la Utawala na kamanda mkuu wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ameamuru kusonga mbele kuelekea magharibi mwa Darfur.
-
AU yatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa kushughulikia mgogoro wa Mali
Nov 10, 2025 07:30Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssef, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa kasi hali ya usalama nchini Mali, ambako makundi aliyoyataja kuwa ya "kigaidi" yamezuia operesheni za kuwasilisha mahitaji ya msingi na hivyo kuzidisha mgogoro wa binadamu unaowakabili raia, pamoja na kuongezeka kwa utekaji nyara.
-
RSF imezika kwa halaiki na kuchoma moto maiti za mamia ya raia El-Fasher kuficha jinai za mauaji ya kimbari
Nov 10, 2025 02:48Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa, maiti za mamia ya raia zimezikwa katika makaburi ya pamoja na nyingine zimechomwa moto na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) mjini El-Fasher magharibi mwa nchi hiyo.