-
Mousavi: Iran haijatoa ahadi yoyote kuhusiana na kuachiwa meli ya mafuta ya "Grace 1"
Aug 16, 2019 10:17Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haijatoa ahadi yoyote kwa ajili ya kuachiwa meli ya mafuta ya "Grace 1" iliyokuwa ikishikilIwa na Waingereza katika eneo la Gibraltar.
-
Imam wa Ijumaa Tehran: Mapambano ya Wayemeni yatawashinda wavamizi
Aug 16, 2019 08:18Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amepongeza mapambano ya watu wa Yemen dhidi ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, mapambano ya Waislamu wa Yemen yatawashinda wavamizi hao.
-
Kamanda Khanzadi awaambia maadui: Ondokeni Ghuba ya Uajemi au mtaondoka kwa madhila
Aug 15, 2019 07:06Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa majeshi ya adui wa Iran yaliyoko katika Ghuba ya Uajemi yanapaswa kuondoka haraka iwezekanavyo katika eneo hilo la sivyo yataondoka kwa madhila.
-
Ayatullah Araki afanya mazungumzo na Sheikh Ibrahim Zakzaky
Aug 15, 2019 05:50Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu mapema leo amefanya mazungumzo ya simu na Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky aliyepelekwa India kwa ajili ya matibabu.
-
Uungaji mkono wa Shekhe wa Muqawama kwa diplomasia ya Zarif
Aug 15, 2019 03:26Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amemtumia ujumbe Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo sambamba na kulaani hatua ya Marekani ya kumwekea vikwazo Mohammad Javad Zarif amesisitizia mshikamano wa muqawama kwa mwanadiplomasia huyo.
-
Mousavi: Iran inaunga mkono Yemen iliyoungana
Aug 14, 2019 21:12Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria matukio ya hivi karibuni ya kusini mwa Yemen na kusema: "Iran imekuwa ikiunga mkono 'Yemen moja iliyoungana' na kulinda umoja wa nchi hiyo ni jukumu la Wayemeni wote."
-
Rais Rouhani: Kudhamini usalama wa Ghuba ya Uajemi hakuhitajii vikosi vya kigeni
Aug 14, 2019 08:21Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, ili kudhamini usalama na utulivu katika Ghuba ya Uajemi hakuna haja ya kuweko vikosi vya kieneo katika eneo hilo.
-
Spika Larijani: Njama za Wazayuni za kuzigawanya nchi za Kiislamu zimegonga mwamba
Aug 14, 2019 08:19Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mkono wa pongezi na baraka kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Hizbullah ya Lebanon katika vita vya siku 33 na kusisitiza kwamba, njama za Wazayuni za kuzigawanya nchi za Kiislamu zimegonga mwamba.
-
Sisitizo la Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu udharura wa kusimama kidete kukabiliana na njama ya kuigawanya Yemen
Aug 14, 2019 07:00Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema, Saudi Arabia na Imarati zinataka kuigawanya Yemen; na akasisitiza kwamba: Inalazimu kusimama na kukabiliana kwa nguvu zote na njama hiyo na kuunga mkono kuwepo Yemen moja, iliyoungana na yenye ardhi yake yote kamili.
-
Iran: Uingereza inatarajiwa baada ya muda si mrefu kuiachia meli ya mafuta iliyoizuia
Aug 13, 2019 22:06Shirika la Bandari na Safari za Majini la Iran limesema, Uingereza inatazamiwa baada ya muda si mrefu kuiachia meli ya mafuta inayomilikiwa na Iran ambayo iliizuia kinyume cha sheria mwezi uliopita katika pwani ya Gibraltar, baada ya pande mbili kubadilishana baadhi ya nyaraka ili kurahisisha kuachiwa kwa meli hiyo.