-
Iran na Misri zataka kusitishwa vita mara moja Ghaza
Jun 02, 2025 23:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, ametoa mwito wa kusitishwa haraka mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza na kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wananchi wa Ukanda huo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akutana na Rais wa Misri jijini Cairo
Jun 02, 2025 08:11Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana leo Jumatatu na Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri jijini Cairo.
-
Naeem Qassem: Misingi ya Imam Khomeini itaendelea kuwa mwanga wa njia ya mapambano
Jun 02, 2025 07:58Sheikh Naeem Qassem, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, amesisitiza kuwa mafundisho ya Uislamu asili wa Mtume Muhammad kupitia misingi ya kimapinduzi ya Imam Ruhullah Khomeini (Mwenyezi Mungu Amrehemu) yataendelea kuwa mwanga unaoongoza harakati za mapambano au Muqawama na vuguvugu za ukombozi katika eneo la Asia na ulimwengu mzima wa Kiislamu.
-
Eslami: Urutubishaji wa madini ya urani ni mstari mwekundu kwa Iran
Jun 02, 2025 07:43Mkuu wa Shirika la Nguvu za Atomiki la Iran (AEOI), Mohammad Eslami, amesema kwa msisitizo kuwa urutubishaji wa madini ya urani ni jambo la msingi lisilojadiliwa katika sera za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akilitaja kuwa ni "mstari mwekundu" kwa taifa.
-
Sera ya vikwazo yakwama, Marekani yasitisha vikwazo vipya dhidi ya Iran
Jun 02, 2025 07:35Serikali ya Marekani imesitisha hatua za kuanzisha vikwazo vipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, jambo linaloashiria kufeli licha ya kampeni ya vikwazo ya mashinikizo ya juu kabisa ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa muda mrefu dhidi ya Iran.
-
Waziri Araghchi yupo Misri kujadili Gaza, uhusiano wa Tehran-Cairo
Jun 02, 2025 03:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi yuko katika mji mkuu wa Misri, Cairo, kwa ajili ya kufanya mazungumzo na maafisa wakuu wa nchi hiyo, juu ya uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu na Misri pamoja na maendeleo katika eneo la Asia Magharibi, yakiwemo mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza.
-
Jeshi la Anga la Iran liko imara kuilinda nchi kwa nguvu zote
Jun 01, 2025 23:28Kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIAF), Brigedia Jenerali Hamid Vahedi amesema kuwa, jeshi hilo liko imara na limejiandaa kikamilifu kulinda anga ya Jamhuri ya Kiislamu kwa hali yoyote ile.
-
Iran yatumia teknolojia ya nyuklia kuzalisha mpunga wakati wa ukame
Jun 01, 2025 06:40Uzalishaji wa mpunga aina ya "Kian" ni mafanikio mapya ya matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia nchini Iran. Mpunga huo unastahamili ukame usio na kifani na hilo ni suluhisho la kisayansi la kukabiliana na tatizo la maji katika mashamba ya mpunga.
-
Jibu la Iran kwa madai ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki
Jun 01, 2025 04:10Wizara ya Mambo ya Nje na Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran zimejibu katika taarifa ya pamoja madai yasiyo na msingi na ya kisiasa ya hivi karibuni ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA .
-
Iran: Ripoti ya IAEA imetolewa kwa mujibu wa matashi ya kisiasa
Jun 01, 2025 03:49Iran imetoa wito kwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kuakisi hali halisi kuhusu mpango wa amani wa nishati ya nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu na kujiepusha na matashi ya kisiasa kwenye ufuatiliaji wake wa shughuli za nyuklia za nchi hii.