-
Eslami aitaka IAEA kutoegemea upande wowote katika mazungumzo ya kati ya Tehran na Washington
Apr 17, 2025 23:09Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa Tehran inataraji kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hautoegemea upande wowote kuhusiana na mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington.
-
Waziri wa Ulinzi wa Saudia yupo Tehran kujadili uhusiano wa pande mbili, masuala ya kieneo
Apr 17, 2025 10:05Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Khalid bin Salman Aal-Saud amewasili Tehran leo Alkhamisi kwa ziara muhimu inayolenga kuimarisha uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Riyadh, na kujadili masuala ya kieneo.
-
Araghchi: IAEA inaweza kutatua kwa amani faili la nyuklia la Iran
Apr 17, 2025 09:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Sayyid Abbas Araghchi amesema Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unaweza kuwa na nafasi na jukumu muhimu katika utatuzi wa amani wa suala la nyuklia la Jamhuri ya Kiislamu.
-
Grossi asisitiza nafasi ya diplomasia katika suala la nyuklia la Iran
Apr 17, 2025 09:13Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), aliwasili Tehran Jumatano, Aprili 16, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Sayyid Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, na Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran.
-
Iran na China ni ngome isiyoweza kupenywa na vikwazo vya Marekani
Apr 17, 2025 02:13Wizara ya Fedha ya Marekani imezidisha mashinikizo dhidi ya Tehran kwa kukiwekea vikwazo kiwanda cha kusafisha mafuta cha China kwa madai ya kununua mafuta ya Iran. Hata hivyo, takwimu zinaonyesha kuwa si tu vikwazo hivyo havijazuia mauzo ya mafuta ya Iran, bali pia vimezidisha ushirikiano wa kiuchumi na kijiografia kati ya Iran na China.
-
Gharibabadi: Iran haina haja ya kupoteza muda kwenye mazungumzo
Apr 17, 2025 02:12Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayehusika na Sheria na Masuala ya Kimataifa amesema kuwa duru ijayo ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani itafanyika kama ilivyopangwa na kwamba Tehran haina haja ya kupoteza muda.
-
Baghaei: Misimamo inayogongana ya Marekani ni ishara ya kutokuwa na nia njema na ya dhati katika mazungumzo
Apr 17, 2025 00:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Esmail Baghei ametoa mjibizo kwa msimamo wenye mgongano ulioonyeshwa na Steve Witkoff, mjumbe maalumu wa Rais wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati na mwakilishi wa nchi hiyo katika mazungumzo na Iran.
-
Iran: Urutubishaji urani 'haujadiliki', mazungumzo chini ya mashinikizo hayatakuwa na tija
Apr 16, 2025 08:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema urutubishaji wa madini ya urani ukiwa ni sehemu ya mpango wa amani wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu "haujadiliki" na kwamba mazungumzo ya Tehran na Washington hayatazaa matunda ikiwa yatafanyika kwa mashinikizo na bila ya pande mbil kuheshimiana.
-
Taratibu ambazo Iran inaona zinahitajika ili kurekebisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa
Apr 16, 2025 06:19Kazem Gharibabadi, Naibu Waziri wa Masuala ya Kisheria na Masuala ya Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amewasilisha mapendekezo ya Jamhuri ya Kiislamu kwa wajumbe wa Kundi la Marafiki wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa katika kikao cha tatu cha Waratibu wa Kitaifa wa Hati ya Marafiki wa Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na Moscow.
-
IRGC: Usalama wa taifa na uwezo wa kijeshi wa Iran ni 'mistari myekundu, haijadiliki'
Apr 15, 2025 23:45Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa, usalama wa taifa na uwezo wa kijeshi wa Iran hauwezi kujadiliwa kwa namna yoyote ile.