Mamluki wengine wawili wa Mossad watiwa nguvuni kaskazini mashariki mwa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128598-mamluki_wengine_wawili_wa_mossad_watiwa_nguvuni_kaskazini_mashariki_mwa_iran
Askari usalama wa Iran wamewatia nguvuni magaidi wawili wa Shirika la Ujasusi la Israel (MOSSAD) katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Khorasan ya Kaskazini, unaopatikana kaskazini mashariki mwa nchi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 22, 2025 01:01 UTC
  • Mamluki wengine wawili wa Mossad watiwa nguvuni kaskazini mashariki mwa Iran

Askari usalama wa Iran wamewatia nguvuni magaidi wawili wa Shirika la Ujasusi la Israel (MOSSAD) katika mkoa wa kaskazini mashariki wa Khorasan ya Kaskazini, unaopatikana kaskazini mashariki mwa nchi.

Javad Ilali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali wa mkoa wa Khorasan Kaskazini jana alieleza kuwa mfumo wa mahakama mkoani humo umedhamiria kwa dhati kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya ujasusi.

Ameongeza kuwa, watu 15 wanahojiwa katika mkoa huo kwa tuhuma za kueneza taarifa za uwongo na propaganda dhidi ya Iran wakati wa vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. 

Mwezi uliopita, wanaume watatu waliopatikana na hatia ya kushirikiana na MOSSAD na kuingiza Iran mabomu ili kuwauwa shakhsia watajika, walinyongwa hapa. 

Katika wiki za karibuni Iran imewatia mbaroni mamia ya mamluki wa shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel MOSSAD. Askari usalama wa Iran pia wamefanikiwa kusambaratisha karakana kadhaa za chini ya ardhi zilizokuwa zikiendeshwa na mamluki wa MOSSAD. 

Washukiwa waliokamatwa wanatuhumiwa kupanga njama ya kutumia ndege ndogo zisizo na rubani, kutengeneza mabomu, kupeleleza maeneo ya kijeshi na kutuma taarifa nyeti kwa utawala wa Israel.