Baqaei: Iran inaunga mkono kuimarisha uhusiano wa kikanda
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128586-baqaei_iran_inaunga_mkono_kuimarisha_uhusiano_wa_kikanda
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo katika mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki hapa Tehran kwamba: Tehran inaunga mkono kukuza uhusiano na nchi za kanda hii, lakini wakati huo huo, imekuwa ikisisitiza kuwa kuanzishwa vivuko na njia mbalimbali hakupasi kuathiri mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Iran.
(last modified 2025-07-21T10:00:26+00:00 )
Jul 21, 2025 10:00 UTC
  • Baqaei: Iran inaunga mkono kuimarisha uhusiano wa kikanda

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo katika mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki hapa Tehran kwamba: Tehran inaunga mkono kukuza uhusiano na nchi za kanda hii, lakini wakati huo huo, imekuwa ikisisitiza kuwa kuanzishwa vivuko na njia mbalimbali hakupasi kuathiri mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Iran.

Esmail Baqaei amesema, kwa miaka miaka miwili sasa tunashuhudia mauaji makubwa ya kimbari katika Ukanda wa Gaza na kilichoongezwa katika mkakati huu wa mauaji ni matumizi ya chakula na maji kama silaha ya kuulia wanawake, watoto na wanaume wa Gaza.  

Amesema, Gaza inazingirwa kwa zaidi ya siku 140; na katika siku mbili tatu zilizopita, tumeshuhudia kilio cha watu wa Palestina kwenye mitandao ya kijamii. Hakuna shehena yoyote ya chakula au dawa iliyoingia Gaza hadi sasa.

Katika muda wa saa 24 watu wa Gaza wasio na hatia karibu 150 wameuawa shahidi katika safu za kupokea msaada wa chakula kutoka kwa kile kinachojulikana kama Taasisi Isiyo ya Kiserikali inayosimamiwa na wakandarasi wa Marekani.  

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa: "Israel inawauwa Wapalestina walioko katika safu za kusubiri mikate. Hakuna maneno yanayoweza kuelezea unyama na ukubwa wa jinai hii", amesema Esmail Baqaei.  

Vilevile amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa uungaji mkono wa Marekani kwa uvamizi wa kijeshi wa Israel dhidi ya Iran na kuitaka Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuitisha kikao maalumu kujadili suala hilo.