-
Iran: Tutatumia njia zote kuuwajibisha utawala wa Kizayuni kwa kuushambulia ubalozi wetu
Apr 02, 2025 08:29Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya jinai iliyofanywa na utawala wa Kizayuni ya kuushambulia ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu mjini Damascus na kutangaza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimia kutumia fursa na njia zote kutekeleza uadilifu na kuuwajibisha utawala wa kigaidi wa Israel.
-
Araqchi: Iran haina lengo la kumiliki silaha za nyuklia
Apr 02, 2025 03:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitaki kuunda na kumiliki silaha za nyuklia kwa hali yoyote ile.
-
Iran yaalani vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon
Apr 02, 2025 03:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Dhahiya katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
-
Rais wa Iran: Waislamu wanapaswa kuwa na mchango athirifu katika kukabiliana na watendajinai duniani
Apr 01, 2025 11:48Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na viongozi wa nchi mbalimbali, akiwapongeza kwa mnasaba wa kusherehekea sikukuu ya Idul-Fitr. Amesisitiza ulazima wa kuimarishwa zaidi umoja na uhusiano wa kindugu baina ya nchi za Waislamu na ulazima wa kuzima njama za maadui.
-
Araghchi: Maadui watajuta kwa kutoa vitisho dhidi ya Iran
Apr 01, 2025 08:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haitamruhusu mtu yeyote kuzungumza nayo kwa lugha ya ubabe na vitisho, akiwaonya maadui kwamba watajuta kulitishia taifa hili.
-
Wizara ya Ulinzi ya Iran: Chokochoko dhidi yetu zitakabiliwa na jibu madhubuti
Apr 01, 2025 07:23Wizara ya Ulinzi ya Iran imewaonya vikali maadui kwamba, kitendo chochote cha uchokozi dhidi ya taifa hili kitakabiliwa na jibu la haraka na madhubuti.
-
Mshauri: Ikiwa Marekani itafanya kosa, Iran itaunda silaha za Nyuklia
Apr 01, 2025 04:16Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, iwapo Marekani itafanya 'kosa' lolote, Iran italazimika, kwa mashinikizo ya wananchi wake, kuelekea kwenye uundaji wa silaha za nyuklia.
-
Iran yalaani vikali vitisho vya Trump vya mashambulizi ya kijeshi
Apr 01, 2025 04:14Iran imelaani vikali vitisho vya hivi karibuni vya Rais wa Marekani, Donald Trump, vya kuishambulia nchi hii kijeshi ambapo imeviitaja kuwa ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na misingi ya Hati ya Umoja wa Mataifa.
-
National Interest: Mji wa makombora wa Iran unaonyesha nguvu ya nchi hiyo
Mar 31, 2025 23:16Gazeti la Marekani la National Interest limeuchambua mji mpya wa makombora wa Iran na kusisitiza kwamba, kufichuliwa mji huo huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika Bahari Nyekundu na Asia Magharibi, ni ujumbe kwa Marekani na maadui wa Iran.National Interest imekiri katika ripoti yake kwamba hifadhi ya makombora ya Iran imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Iran inanyoosha mkono wa udugu kwa mataifa yote ya Kiislamu
Mar 31, 2025 08:43Mapema leo Jumatatu, katika kikao na viongozi wa serikali, mabalozi wa nchi za Kiislamu na matabaka tofauti ya wananchi wa Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya kislamu, Imam Ali Khamenei amesema kuimarika heshima ya Uislamu na kukabiliana na dhulma na uonevu wa madola makubwa vinategemea umoja na utambuzi wa Umma wa Kiislamu.