-
Baqaei: Marekani ijitayarishe kwa athari za hatua yoyote dhidi ya Iran
Mar 31, 2025 08:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametangaza katika ujumbe wake kwamba, tishio lolote la rais wa nchi la kuishambulia Iran kwa mabomu ni ukiukaji wa wazi na kiini cha amani na usalama wa kimataifa.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Utawala fisadi wa Israel ni ‘kikosi cha niaba tu’ katika eneo, ni lazima ung'olewe
Mar 31, 2025 03:49Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, kikosi pekee cha niaba katika eneo hili ni utawala wa Kizayuni ambao unavamia nchi nyingine kwa niaba ya madola ya kikoloni ya dunia na ni "lazima ung'olewe."
-
Rais wa Iran atoa mkono wa Idi kwa viongozi na wananchi wa mataifa ya Kiislamu
Mar 30, 2025 23:51Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia salamu za mkono wa Idi na kuwapongeza viongozi na wananchi wa mataifa ya Kiislamu kwa mnasaba wa kuadhimisha na kushereheka Idul-Fitri, siku ya sherehe na furaha kubwa kwa Waislamu.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran atoa wito wa umoja katika ujumbe wa Idul Fitr
Mar 30, 2025 23:11Katika ujumbe wa pongezi kwa wenzake Waislamu kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Fitr, inayoadhimisha baada ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa wito wa kuimarisha zaidi umoja na huruma miongoni mwa mataifa ya Kiislamu.
-
Rais wa Iran: Mwelekeo wa mazungumzo unategemea mwenendo wa Wamarekani
Mar 30, 2025 23:11Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran haijawahi kukwepa mazungumzo, lakini ni aina ya mwenendo wa Wamarekani ndio unaoamua ikiwa mazungumzo yataendelea au la.
-
Majeshi ya Iran yaahidi ‘Majibu Makali’ kwa tishio lolote
Mar 30, 2025 23:11Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema iko tayari kutoa jibu kali na lenye nguvu dhidi ya tishio lolote, uchokozi, au uvamizi maadui.
-
Kamanda: Iran ina uwezo wa kupiga ngome za adui popote pale
Mar 30, 2025 03:58Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Admeli Alireza Tangsiri amesema kwa mara nyingine tena kuwa, uwezo wa kijeshi wa Iran ni wa kipekee, huku akionya dhidi ya vitisho akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu haiwezi kufanya mazungumzo na yeyote kuhusu maghala yake ya makombora.
-
Araqchi: Mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Yemen yanadhihirisha namna nchi hiyo inavyoshiriki katika uvunjaji wa sheria wa Israel
Mar 30, 2025 03:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amelaani mashambulizi ya kijeshi ya mara kwa mara ya Marekani katika maeneo mbalimbali ya Yemen na kusema: Mashambulizi ya kijeshi ya Marekani huko Yemen sambamba na kushtadi mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na hujuma zake dhidi ya Lebanon na Syria, yanaonyesha namna Marekani inavyoshiriki katika uvunjaji sheria wa Israel na kwenda sambamba na utawala huo katika kueneza machafuko na hali ya mchafukoge katika eneo.
-
Azma ya Iran ya kutekeleza operesheni ya tatu ya kijeshi dhidi ya Israel
Mar 29, 2025 04:25Mshauri mwandamizi wa kijeshi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei amethibitisha kwamba Iran itatekeleza operesheni ya tatu ya kijeshi dhidi ya utawala wa Israel katika kujibu vitendo vya uchokozi vya utawala huo dhidi ya Iran.
-
Iran yalaani shambulio la anga la Israel dhidi ya Beirut
Mar 29, 2025 04:25Iran imelaani vikali shambulio kubwa la anga la utawala haramu Israel kwenye maeneo ya makazi katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalifikiwa kati ya utawala huo na harakati ya Muqawama ya Lebanon, Hizbullah.