-
Qalibaf: Utawala wa Kizayuni ni mtambo wa mauaji wa Marekani mtendajinai
Mar 28, 2025 23:43Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Utawala wa Kizayuni wa Israel ni mashine ya mauaji ya Marekani mtendajinai."
-
Azimio la Siku ya Kimataifa ya Quds: Tutakabiliana na uhasama wa Marekani na kuihami Palestina
Mar 28, 2025 11:23Washiriki katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds wamesisitiza udharura wa kukabiliana vikali na uhasama wa Marekani na kuunga mkono malengo ya mapambano ya ukombozi wa Palestina.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa: Maandamano ya Siku ya Quds ni dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mungu
Mar 28, 2025 09:31Imam wa Swala ya Ijumaa ya leo katika mji wa Tehran ameashiria kushiriki kwa wingi na kwa hamas wananchi wa Iran ya Kiislamu katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu na kusema: Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds siku zote yamekuwa dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mwenyezi Mungu.
-
Jibu la Iran kwa barua ya Trump/ Araqchi: Mazungumzo chini ya mashinikizo hayana maana
Mar 28, 2025 08:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Iran amesisitiza kwamba mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa nchi hiyo hayana maana maadamu sera ya "shinikizo la juu" na vitisho vya kijeshi bado vipo.
-
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Mar 28, 2025 07:54Mnamo mwaka 1979, mara tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa siku ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, akiwa amesimama imara katika kupigania haki za watu wote wanaodhulumiwa ulimwenguni.
-
Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Mar 28, 2025 04:15Wananchi Waislamu wa Iran kote nchini wamejitokeza kwa mamilioni kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kuonyesha mshikamano na Palestina, na kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
-
Kiongozi Muadhamu: Siku ya Quds ya mwaka huu itakuwa ya aina yake
Mar 27, 2025 23:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu yanayofanyika leo Ijumaa ya Machi 28 kote duniani yana umuhimu mkubwa kuliko miaka iliyopita.
-
Marajii Taqlidi na Maulamaa watoa wito wa kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Mar 27, 2025 22:59Marajii Taqlidi na Maulamaa nchini Iran wamesisitiza juu ya kushiriki pakubwa na kwa hamasa wananchi katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya quds.
-
Iran, Lebanon, Iraq, Yemen zaanza luteka ya kuwaunga mkono Wapalestina Gaza
Mar 27, 2025 08:00Vikosi vya Baharini vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na vikosi kutoka Lebanon, Iraq na Yemen, vinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya majini katika 'maonyesho ya nguvu' dhidi ya Israel na kutangaza mshikamano na Wapalestina huko Gaza.
-
Tehran yaihutubu EU: Shughulikieni jinai za Israel badala ya kutoa madai ya kinafiki
Mar 27, 2025 07:38Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baghaei amemkosoa vikali mkuu mpya wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, kutokana na matamshi yake ya karibuni ya kuitaja Iran kama "tishio" wakati wa ziara yake ya karibuni katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.