-
Iran: Hatuchukui maagizo kutoka kwa yeyote kuhusu teknolojia ya nyuklia
Mar 11, 2025 08:30Makamu wa Kwanza wa Rais, Mohammad Reza Aref amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko imara katika sera yake huru ya nyuklia na wala haishauriani au kuchukua maagizo kutoka kwa mtu yeyote yule.
-
Jibu la msingi la Iran kwa hatua haramu ya Marekani mkabala wa Iraq; Araqchi aikosoa Marekani
Mar 11, 2025 03:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuhusu dhamira ya nchi hii kwa Iraq ili kutoa ushirikiano kwa ajili ya kukomesha hatua za Marekani zilizo kinyume cha sheria.
-
"Mantiki ya Muqawama ya IRGC ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu"
Mar 11, 2025 01:09Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami amesema mantiki ya Muqawama ya SEPAH ndiyo njia pekee ya kuwaokoa Waislamu mkabala wa kutawaliwa na maadui.
-
Meli za kivita za Russia na China zafika Iran kwa mazoezi makubwa ya pamoja ya kijeshi
Mar 11, 2025 00:59Meli za kivita za Russia na China zimewasili katika maji ya eneo la Iran kaskazini mwa Bahari ya Hindi kushiriki katika mazoezi makubwa ya pamoja ya wanamaji yanayojulikana kama Mkanda wa Usalama 2025 (Security Belt-2025), ambayo yatashirikisha vitengo mbalimbali kutoka mataifa haya matatu yenye nguvu za kijeshi.
-
Iran yakemea mauaji ya waliowachache nchini Syria, yataka yakomeshwe
Mar 11, 2025 00:54Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa tamko kali la kulaani mauaji ya raia nchini Syria, ikielezea machafuko hayo kuwa ni umwagaji damu usiokubalika pamoja na vitendo vyovyote vya uhasama vinavyolenga makundi ya wachache katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Iran: Kuna tofauti kati ya mazungumzo na vitisho
Mar 10, 2025 08:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema katu Jamhuri ya Kiislamu haitafanya mazungumzo kuhusu mradi wake wa nishati ya nyuklia chini ya mashinikizo, kwani mazungumzo ni tofauti na utumiaji wa mabavu na vitisho.
-
Iran yalaani kufutwa mkutano wa Geneva wa kuijadili Palestina
Mar 10, 2025 07:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amekosoa vikali uamuzi wa Uswisi wa kufuta Kongamano la Hati ya Geneva kuhusu Palestina.
-
Rais wa Iran: Machafuko na migogoro ni hatari kwa nchi za Asia na dunia
Mar 10, 2025 03:30Rais Masoud Pezeshkian amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatambua mvutano wowote, machafuko na migogoro kuwa ni hatari kwa eneo la Asia Magharibi na dunia nzima kwa ujumla."
-
Iran: Haitatokea katu kufanywa mazungumzo ya kuufumua mpango wetu wa nyuklia
Mar 09, 2025 23:38Ofisi ya Uwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa imetangaza kwamba ikiwa lengo la kutaka kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ni "kuufumua mpango wa amani wa nyuklia wa Iran," mazungumzo kama hayo hayatafanyika katu.
-
Qalibaf: Iran haitasubiri barua yoyote kutoka Marekani
Mar 09, 2025 07:57Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema Jamhuri ya Kiislamu haisubiri barua yoyote kutoka kwa Marekani, kwani taifa hili linategemea uwezo wa ndani katika kukabiliana na changamoto zake.