-
Abu Sharif: Irada ya muqawama ina nguvu kuliko njama yoyote
Sep 30, 2024 08:31Mwakilishi wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema baada ya utawalal wa Kizayuni kumuua shahidi Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kwamba: Licha ya kuipoteza nembo hiyo adhimu, lakini si tu muqawama hautadhoofishwa bali utaendeleza njia yake kwa nguvu zaidi na kwa azma kamili.
-
Subirini; jibu la kamanda wa jeshi la Iran kuhusu radiamali ya Tehran kwa mauaji ya shahidi Nasrullah
Sep 30, 2024 07:49Kamanda mkuu wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu radiamali ya Iran na mhimili wa muqawama kwa mauaji ya Sayyid Hassan Nasrullah kuwa, subirini.
-
Tume ya Haki za Binadamu ya Iran yatoa taarifa kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon
Sep 30, 2024 07:44Tume ya Haki za Binadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa ikilaani shambulio la kigaidi la utawala katili na unaotenda jinai wa Kizayuni katika eneo la Dhahiya kusini mwa Beirut, mji mkuu wa Lebanon lililowauwa shahidi shakhsia watajika wa muqawama pamoja na mujahid Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.
-
Rais Pezeshkian: Jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel hazitabaki bila kujibiwa
Sep 30, 2024 04:39Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema ni lazima Tehran itoe jibu kwa utawala unaotenda jinai wa Israel.
-
Rekodi mpya katika uzalishaji wa umeme wa nyuklia nchini Iran
Sep 30, 2024 04:32Kiwanda pekee cha nishati ya nyuklia cha Iran kilifikia kiwango cha uzalishaji cha zaidi ya saa bilioni 7 za kilowati katika mwaka huu wa Hijria Shamsiya.
-
Kamanda Qaani: Tutakuwa bega kwa bega na Hizbullah hadi Quds na Palestina zitakapokombolewa
Sep 30, 2024 00:00Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, Iran itakuwa bega kwa bega na harakati ya Muqawama ya Lebanon ya Hizbullah hadi ukombozi wa Palestina na Quds Tukufu.
-
Utayarifu na uwezo wa Iran wa kukabiliana na migogoro inayoibuliwa na utawala wa Kizayuni na Marekani
Sep 29, 2024 08:29Sayyid Abbas Araghchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika kikao na Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametoa onyo kali kuhusu hatua za utawala wa Kizayuni na Marekani za kuibua migogoro mipya katika eneo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Baraza la Usalama linapaswa kuchukua hatua kukomesha jinai za Israel
Sep 29, 2024 07:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa heshima na hadhi ya Umoja wa Mataifa imeharibiwa vibaya isipokuwa kama Baraza la Usalama litachukua hatua za haraka kukomesha uchokozi wa utawala ghasibu wa Israel.
-
SEPAH: Malengo matukufu ya ukombozi wa Quds yamekaribia kufikiwa
Sep 29, 2024 02:40Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) ametoa ujumbe maalumu wa pongezi na wa mkono wa pole kufuatia kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na kusisitiza kuwa, malengo matukufu ya ukombozi wa Quds yamekaribia kufikiwa na historia itathibitisha hilo.
-
Ghalibaf: Sayyid Hassan Nasrullahh ameuawa shahidi katika njia ya ukombozi wa Quds
Sep 29, 2024 02:40Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameuawa shahidi katika njia takatifu ya kuupigania Uislamu na ukombozi wa Quds.