-
Iran yazitaka nchi za Kiislamu kuungana kukomesha jinai za utawala wa Kizayuni
Sep 29, 2024 02:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa nchi za Kiislamu zina wajibu wa kuungana na kushikamana katika kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni huko Palestina na Lebanon.
-
Ayatullah Khamenei: Vipigo vya Muqawama dhidi ya utawala unaozidi kunyauka wa Kizayuni vitakuwa shadidi
Sep 28, 2024 22:47Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, akisisitiza kuwa: Njia ya mapambano ya Sayyid wa Muqawama itaendelea na mashambulizi ya Kambi ya Muqawama yatakuwa shadidi zaidi kwenye kiwiliwili kilichochakaa na kinachoeleka kuangamia cha utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais Pezeshkian: Kuuawa shahidi Sayyid Nasrullah kunaimarisha zaidi Muqawama
Sep 28, 2024 12:11Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuuawa shahidi watu mashuhuri wa Kambi ya Muqawama, akiwemo kiongozi wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah, kunaimarisha zaidi mti wa mwema wa Muqawama na mapambano, na kuongeza kuwa: "Ulimwengu hautasahau kwamba amri ya shambulio hilo la kigaidi imetolewa New York."
-
Ombi la Iran kwa BRICS
Sep 28, 2024 08:02Kuacha kutumia sarafu ya dola, kukabiliana na vikwazo vya upande mmoja vya nchi za Magharibi, kuwa na sekretarieti ndogo na ya haraka na kufanyika vikao vya BRICS katika nchi wanachama kwa mujibu wa hali ya kijiografia, ni matakwa manne yaliyowasilishwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa kundi la BRICS pambizoni mwa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Wazayuni si lolote si chochote kuweza kuisababishia madhara makubwa Hizbullah
Sep 28, 2024 07:24Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kuwa, watenda jinai wa Kizayuni wajue kwamba wao si lolote kuweza kuusababishia madhara makubwa muundo imara wa Hizbullah ya Lebanon.
-
Iran: Marekani ni muungaji mkono mkuu na mshirika wa jinai za Israel
Sep 27, 2024 10:13Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, Marekani ndio mshirika muhimu zaidi katika jinai za kivita za utawala ghasibu wa Israel katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina na jinai zinazoendelea dhidi ya taifa la Lebanon.
-
Ayatullah Khatami: Kuundwe asasi ya kweli ya haki za binadamu kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni
Sep 27, 2024 09:47Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza udharura wa kuundwa taasisi ya kweli ya haki za binadamu kwa ajili ya kuchunguza jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na katika maeneo mengine ya Palestina.
-
Sisitizo la Pezeshkian la haja ya kuondolewa vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Iran
Sep 27, 2024 08:28Moja ya iliyokuwa mada muhimu katika hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ilikuwa ni ulazima wa kuondolewa vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na kujiweka mbali na mtazamo wenye mwelekeo wa vitisho katika maingiliano na mashirikiano ya kimataifa.
-
Iran: Usalama na amani ya Lebanon ni muhimu sana kwetu
Sep 27, 2024 03:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aemsema kuwa, ni jambo lililo wazi kabisa kwamba Jamhuri ya Kiislamu haiwezi kukaa kimya mbele ya vita vikubwa na vya pande zetu nchini Lebanon.
-
Rais wa Iran: Nchi za Kiislamu zikate uhusiano wa kiuchumi na Israel
Sep 26, 2024 08:27Rais wa Iran amesema, kama nchi za Kiislamu zitakata uhusiano wa kiuchumi na utawala wa Israel unaotekeleza mauaji ya kimbari, utawala huo unaouwa watoto hautaweza tena kutenda jinai na uvamizi.