-
Raisi: Kukata uhusiano wa kiuchumi na utawala wa Kizayuni ni suluhisho la kivitendo la kukomesha jinai za Israel
Mar 03, 2024 01:10Seyyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo na Rais wa Iraq, Abdul Latif Rashid kwamba, kukata uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na utawala wa Kizayuni wa Israel ni suluhisho la kivitendo la kukomesha jinai za Wazayuni.
-
Waziri: Uzalishaji wa gesi ya Iran umeongezeka licha ya vikwazo
Mar 03, 2024 01:09Waziri wa Mafuta wa Iran amesema uzalishaji wa gesi ya Jamhuri ya Kiislamu umeendelea kuongezeka siku baada ya siku, licha ya vikwazo vya Wamagharibi dhidi ya sekta ya nishati ya taifa hili.
-
Utunishaji misuli; Choopan wa Iran atwaa tuzo ya kifahari
Mar 03, 2024 07:44Mtunishaji misuli veterani wa Iran, Hadi Choopan ametwaa taji la kimataifa la 'Bwana Olympia' katika tuzo za Arnold Classic 2024.
-
Raisi: Afrika ina nafasi muhimu katika sera ya nje ya Iran
Mar 02, 2024 11:40Rais Ebrahim Raisi wa Iran ameeleza kuwa Afrika ina nafasi muhimu katika sere za nje za serikali yake na akasema: "Suala la kuwa na mahusiano na Afrika kwa ujumla, hususan nchi za Kiislamu barani humo lina nafasi ya pekee sana katika sera yetu ya mambo ya nje."
-
Ushiriki wa Wairani katika uchaguzi, jibu kwa misimamo ya uingiliaji kati hasi ya Merekani
Mar 02, 2024 10:11Kushiriki kwa wananchi wa Iran katika uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na Baraza la Wataalamu Wamaomchagua Kiongozi Mkuu, kwa mara nyingine tena, kumezima njama za wapinzani wa Jamhuri ya Kiislamu wakiongozwa na Marekani, za kuwakatisha tamaa wananchi ili wasishiriki katika upigaji kura.
-
Zoezi la kuhesabu kura Iran linaendelea; matokeo yaanza kutangazwa
Mar 02, 2024 04:04Zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na Baraza la Watalaamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran linaendelea.
-
Raisi awasili Algeria kushiriki Mkutano wa Saba wa Nchi za Gesi Duniani
Mar 02, 2024 04:02Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Algiers mji mkuu wa Algeria na kulakiwa katika uwanja wa ndege na Nadir Larbaoui, Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
-
Global Firepower: Iran ni nchi ya 14 kwa nguvu za kijeshi duniani
Mar 02, 2024 04:01Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetajwa kuwa nchi ya 14 duniani kwa nguvu za kijeshi.
-
Raisi: Afrika ina nafasi muhimu katika sera ya kigeni ya serikali
Mar 02, 2024 01:01Rais Seyed Ebrahim Raisi wa Iran amesisitiza kuwa, bara la Afrika lina nafasi muhimu katika sera za kigeni za serikali ya Iran na kuongeza kuwa: "Uhusiano na Afrika kwa ujumla na hasa nchi za Kiislamu barani Afrika una nafasi maalum sana katika sera zetu za kigeni."
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Katiba imepelekea kuongezeka ushiriki wa wananchi katika muundo wa kisiasa wa nchi
Mar 01, 2024 10:50Imamu wa muda na Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema juhudi za kutekeleza katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa umakini zaidi kadiri iwezekanavyo ni moja ya sababu kuu za kuongezeka kiwango cha ushiriki na kupanda nafasi na mchango wa wananchi katika mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.