-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kuitembelea Misri karibuni
Jan 22, 2024 08:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian anataziwa kuitembelea Misri ndani ya siku chache zijazo, huku utawala wa Kizayuni ukiingiwa na kiwewe kutokana na kuendelea kuimarika uhusiano wa Tehran na Cairo.
-
Satalaiti ya Thuraya; nembo nyingine ya uwezo mkubwa wa wasomi vijana wa Iran
Jan 22, 2024 05:38Satalaiti ya Thuraya ambayo imebuniwa na kutengenezwa kwa juhudi na hima ya wasomi vijana wa Iran na kurushwa katika anga za juu, imefanikiwa kutuma taarifa zake za awali na kuthibitisha kuwa imetua sehemu iliyokusudiwa kwa mafanikio makubwa.
-
Raisi: Iran inaunga mkono kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel ICJ
Jan 22, 2024 04:01Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono uamuzi wa 'busara' na wa 'kihistoria' wa Afrika Kusini wa kuwasilisha kesi dhidi ya utawala haramu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), kuhusu jinai za mauaji ya kimbari zinazotekelezwa na utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Satalaiti mpya ya Iran yatuma taarifa za kwanza kabisa ardhini
Jan 21, 2024 23:29Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, satalaiti mpya zaidi ya Iran iitwayo Thuraya imefanikiwa kuunganisha mawasiliano ardhini na kutuma taarifa za awali kabisa.
-
Amir-Abdollahian: Harakati za washauri wa kijeshi wa Iran za kupambana na ugaidi zitaendelea kwa nguvu kamili
Jan 21, 2024 07:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa mjibizo kufuatia kuuawa shahidi washauri watano wa Iran nchini Syria katika shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni na kueleza kwamba: "kushindwa Wazayuni kukabiliana na irada na matakwa ya watu wa Gaza hakutaweza kufidiwa kwa vitendo hivi vya kigaidi."
-
Shambulio la kigaidi la Israel dhidi ya Syria na kuuawa shahidi washauri watano wa Iran
Jan 21, 2024 05:50Washauri watano wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliuawa shahidi jana Jumamosi katika shambulizi la kigaidi la anga lililofanywa na utawala wa Kizayuni huko Damascus, mji mkuu wa Syria.
-
Kan'ani: Kuna uhusiano mkubwa kati ya utawala gaidi wa Israel na Daesh
Jan 21, 2024 04:22Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali jinai na uchokozi uliofanywa mapema jana na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la raia huko al Mezza, Damascus mji mkuu wa Syria na kuuwa shahidi washauri watano wa kijeshi wa Iran na askari kadhaa wa Syria.
-
Iran na Sudan zatilia mkazo kuiunga mkono Palestina
Jan 21, 2024 04:19Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan wameisitiza ulazima wa kuliunga mkono taifa la Palestina mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Raisi: Mauaji ya washauri wa kijeshi wa IRGC hayatapita bila kujibiwa
Jan 21, 2024 00:03Rais Ebrahim Raisi wa Iran amelaani vikali shambulizi la kigaidi la Israel katika mji mkuu wa Syria, Damascus lililopelekea kuuawa shahidi washauri watano wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, vitendo vya aina hiyo vya kioga haviwezi kupita hivi hivi bila kupewa jibu.
-
Washauri 5 wa Iran wauawa shahidi katika shambulio la kigaidi la Israel huko Damascus
Jan 20, 2024 23:13Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limetangaza kuwa washauri wake watano wa kijeshi wameuawa katika shambulizi la kigaidi la Israel katika mji mkuu wa Syria.