-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran: Gaza imekuwa gereza kubwa zaidi la wazi duniani
Jan 20, 2024 10:19Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika kikao cha Harakati ya Nchi Zisizofungamano ya Siasa za Upande Wowote (NAM) kinachofanyika Kampala nchini Uuganda kwamba: Mzingiro wa muda mrefu wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza umelifanya eneo hilo kuwa jela kubwa zaidi ya wazi duniani.
-
New York Times: Iran imetuma ujumbe kwa Israel kwa kombora la Khaybar-Shekan
Jan 20, 2024 09:04Gazeti la Marekani la New York Times limelitaja shambulio la hivi karibuni la makombora ya Iran dhidi ya ngome za kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini Syria kwa kutumia kombora la kisasa la "Khaybar Shekan" kuwa sio tu ni kulipiza kisasi dhidi ya ISIS bali pia ni onyesho la nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya kambi ya Magharibi na hasa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Pakistan yatangaza kurejesha uhusiano kamili na Iran baada ya mivutano iliyojitokeza
Jan 20, 2024 03:23Pakistan imetangaza kurejesha kikamilifu uhusiano wa kidiplomasia na Iran baada ya kujitokeza mivutano mikali ya mpakani ambayo haijawahi kushuhudiwa kati ya nchi mbili juu ya operesheni za kupambana na ugaidi.
-
Magaidi kadhaa wa shambulio la Kerman wauawa, baadhi wakamatwa
Jan 20, 2024 00:33Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imesema vikosi vyake vimefanikiwa kuwaangamiza na kuwatia mbaroni magaidi kadhaa wa shambulio la kigaidi la mapema mwezi huu katika mji wa Kerman, kusini mashariki mwa Iran lililopelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya watu.
-
Azma thabiti ya Iran na Pakistan ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kupambana na ugaidi
Jan 19, 2024 23:30Baada ya kushadidi mivutano ya mpakani kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan katika kipindi cha siku mbili zilizopita, viongozi wa Tehran na Islamabad wamesisitiza kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya nchi mbili, kuheshimiwa umoja wa ardhi za mataifa hayo mawili na kuwepo uratibu na mashauriano ya karibu zaidi katika kupambana na magenge ya kigaidi.
-
Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Operesheni ya IRGC lilikuwa onyo dhidi ya Wazayuni
Jan 19, 2024 10:28Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesema shambulio la makombora la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) dhidi ya kituo kikuu cha ujasusi cha shirika la ujasusi la utawala haramu wa Israel (Mossad) katika eneo la Kurdistan ya Iraq limetoa onyo kali mkabala wa tishio la Wazayuni.
-
Iran yakosoa taarifa ya Arab League, yasema itaendelea kuwaadhibu watenda jinai
Jan 19, 2024 08:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali taarifa ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kufanya shambulio la makombora dhidi ya kituo kikuu cha ujasusi cha shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel Mossad katika eneo la Kurdistan ya Iraq.
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran kushiriki mkutano wa NAM Uganda
Jan 19, 2024 00:01Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kwenda Kampala, mji mkuu wa Uganda kuhudhuria Mkutano wa 19 wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM).
-
Iran yaikosoa US kwa kuiweka Ansarullah katika orodha ya 'ugaidi'
Jan 19, 2024 00:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali hatua ya Marekani ya kuiweka Harakati ya Ansarullah ya Yemen kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi" na kueleza kwamba, kitendo hicho ni katika mfululizo wa hatua za Washington za kuuunga mkono utawala wa kigaidi wa Israel.
-
Balozi mdogo wa Pakistan Tehran aitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
Jan 18, 2024 05:58Balozi mdogo wa Pakistan mjini Tehran ameitwa katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kufuatia mlipuko uliotokea leo asubuhi katika kijiji cha mpakani katika mkoa wa Sistan na Baluchistan hapa nchini.