-
Iran yakosoa msimamo wa Russia kuhusu visiwa vitatu vya Jamhuri ya Kiislamu
Dec 22, 2023 22:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Russia kwamba, Tehran haiwezi kufanya majadiliano na mashauriano yoyote juu ya mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi yote ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Palestina ndiyo kadhia muhimu zaidi ya Umma wa Kiislamu
Dec 22, 2023 08:04Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Palestina ndiyo kadhia muhimu zaidi ya Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Leo hii harakati ya Muqawama ndiye mshindi halisi.
-
Msaada wa Marekani kwa Israel watajwa kuwa sababu kuu ya jinai dhidi ya Wapalestina
Dec 22, 2023 04:37Washiriki katika mkutano wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) wamesisitiza kuwa misaada na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndio sababu kuu ya kuendelea jinai dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Raisi: Ulimwengu umeshangazwa na mapambano ya Wapalestina dhidi ya Israel
Dec 22, 2023 00:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema dunia inashangazwa na Muqawama na mapambano ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala wa haramu wa Israel.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje: Iran haitasita hata kidogo kulinda ardhi yake yote
Dec 21, 2023 08:10Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran haitasita hata kidogo kulinda ardhi yake yote. Nasser Kanani ameeleza haya katika radiamali yake kwa taarifa iliyotolewa na Jukwaa la Ushirikiano wa Kiarabu na Russia kuhusu visiwa vitatu vya Iran.
-
Amir Abdollahian: Marekani inabeba dhima kimataifa kwa kuunga mkono maangamizi ya kizazi yanayofanywa na Israel
Dec 21, 2023 07:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Oman kwamba Marekani inabeba dhima kimataifa kwa kushiriki kwake katika maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya taifa la Palestina.
-
Rais Raisi amwambia Amir wa Kuwait: Palestina ni kadhia nambari moja
Dec 21, 2023 02:46Huku kukiwa na vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, Rais Ebrahim Raisi wa Iran amelitaja suala la Palestina kuwa suala "muhimu zaidi" la Asia Magharibi na dunia nzima.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran azungumza na waziri mwenzake wa Afrika Kusini, Ghaza maudhui kuu
Dec 20, 2023 23:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Afrika Kusini na kujadiliana naye masuala mbalimbali muhimu ya pande mbili, ya kieneo na ya kimataifa na hasa vita vya Ghaza huko Palestina.
-
Ayatullah Ramezani: Sheikh Zakzaky ni mfano halisi wa mujahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu
Dec 20, 2023 11:58Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as) amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na kusema kuwa, Sheikh Zakzaky ni mfano halisi wa Mujahid fi Sabilillah (mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu).
-
Iran: Haiwezekani kabisa kuuvunja nguvu muqawama
Dec 20, 2023 07:44Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, harakati ya muqawama ni uhakika wa kieneo ambao ndio unaoleta utulivu na usalama katika ukanda huu mzima na ndiyo nguvu inayopambana kikweli na vitendo vya kigaidi na magenge ya ukufurishaji.