-
Rais wa Iran afungua Mkutano wa 37 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu
Oct 01, 2023 10:18Kongamano la 37 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu limeanza leo jijini Tehran kwa hotuba ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Serikali ya Sweden lazima iheshimu kanuni za kimsingi za haki za binadamu
Oct 01, 2023 10:16Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Serikali ya Sweden inatakiwa kujibu matakwa ya wazi kabisa ya Waislamu kwa kuwajibika na kufuata kikamilifu kanuni za kimsingi za haki za binadamu, kwa kuhimiza maadili na kuishi pamoja kwa amani wafuasi wa dini tofauti na kuchukua hatua za kivitendo na zenye ufanisi.
-
Iran kujiunga na mfumo wa BRICS PAY ili kukwepa vikwazo vya Marekani
Oct 01, 2023 03:52Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Qalibaf amesema Iran itajiunga na BRICS PAY, mfumo wa kibenki wa kielektroniki unaotumiwa na muungano wa BRICS wa mataifa yanayoinukia kiuchumi, ili kukwepa vizuizi vya kibenki vilivyosababishwa na vikwazo vya Marekani.
-
Nafasi ya juu ya kielimu ya Iran katika nchi za Kiislamu na dunia
Sep 30, 2023 23:07Makamu wa Rais katika Masuala ya Elimu na Teknolojia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Katika kivuli cha siasa za kistratijia za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, hivi sasa Iran ya Kiislamu imebadilika na kuwa nchi mashuhuri kielimu na yenye wasomi wakubwa na mashirika muhimu ya kiteknolojia.
-
Raisi: Magharibi wana wasiwasi wa kukabiliwa na ustaarabu mpya
Sep 30, 2023 12:18Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema katika toleo la tano la Tuzo ya al Mustafa (SAW) kuwa sayansi na elimu yenye manufaa ni elimu inayosababisha saada na ufanisi kwa mwanadamu na kuongeza kuwa, tangu hapo awali, Wamagharibi walikuwa na wasiwasi kwamba kutajitokeza ustaarabu mpya wa kukabiliana nao, na hii ndiyo sababu kuu ya vita dhidi ya Uislamu (Islamophobia) na hujuma dhidi ya Iran (Iranophobia).
-
Iran yatangaza utayari wa kuimarisha uhusiano wake na Tanzania
Sep 30, 2023 04:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuimarisha uhusiano na maelewano ya pande mbili kati yake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-
Satelaiti ya Iran Nour 3, thibitisho la kushindwa vikwazo dhidi ya irada ya wanasayansi wa Iran
Sep 30, 2023 03:25Kupitia ujumbe, rais wa Iran amesema kurushwa katika anga za mbali satelaiti ya Iran Nour 3 kwa kutumia kombora la Qased la Iran ni thibitisho la msemo kwamba "sisi tunaweza" na wakati huo huo ni dhihirisho la kufeli vikwazo dhidi ya irada ya wanasayansi vijana wa Iran.
-
Rais wa Iran alaani mashambulizi pacha ya kigaidi Pakistan
Sep 30, 2023 01:16Rais Ebrahim Raisi wa Iran amelaani mashambulizi mawili ya kigaidi yaliuoua makumi ya watu katika jimbo la kusini magharibi la Balochistan nchini Pakistan.
-
Jeshi la Wanamaji la Iran kujenga kambi ya kudumu barani Antaktika
Sep 29, 2023 09:40Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeri Shahram Irani amedokeza kuwa jeshi hilo lina mpango wa kujenga kituo cha kudumu katika bara la Antaktika, ikiwa ni pamoja na kuanzisha kituo cha kudumu cha harakati za kijeshi na kisayansi.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran asisitiza kuhusu umoja wa Waislamu
Sep 29, 2023 09:40Khatibu wa Sala ya Ijumaa jijini Tehran amesisitiza umuhimu wa umoja wa Waislamu.