Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran asisitiza kuhusu umoja wa Waislamu
Khatibu wa Sala ya Ijumaa jijini Tehran amesisitiza umuhimu wa umoja wa Waislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB; Hujjat-ul-Islam wal-Muslimeen Kadhim Siddiqui Imam muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza ulazima wa kuweko umoja baina ya Waislamu.
Akihutubu katika Sala ya Ijumaa ya wiki hii mjini Tehran amesema: "Shetani ni miongoni mwa vyanzo vya kuvuruga umoja, na Qur'ani Tukufu inamtambulisha Shetani kuwa ndiye chanzo cha mifarakano na migongano. Katika dunia ya leo, shetani mkuu ni Marekani akishirikiana na Uingereza ambayo chanzo cha uovu."
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Hujjatul Islam Siddiqui amegusia hotuba ya hivi karibuni ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Seyed Ebrahim Raisi katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo aliitaja Qur'ani Tukufu kuwa ni kitabu chenye kujenga ustaarabu na binadamu na chimbuko la umoja na kusema: Raiswa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameiarifisha Qur'ani katika Umoja wa Mataifa kama kama chanzo cha nuru."
Hujjat al-Islam na al-Muslimeen Siddiqi, ameashiria kutumwa kwa satelaiti ya Noor 3 ya Iran katika anga za mbali siku ya Jumatano na kusema: Hatua hii ni ukurasa mwingine wa dhahabu katika kitabu cha heshima cha Iran ya Kiislamu.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran amepongeza juhudi za vikosi vya usalama vya Iran katika kuzima makumi ya njama za hujuma za kigaidi nchini hivi karibuni.