-
Iran yakosoa uamuzi wa nchi 3 za Ulaya wa kuendeleza vikwazo
Sep 15, 2023 04:19Iran imelaani uamuzi wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani (E3) wa kuendeleza vikwazo vyao vya makombora ya balistiki na vinavyohusiana na nyuklia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kinyume na makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Tehran na madola sita makubwa ya dunia.
-
Salami: Vitisho dhidi ya Iran vinazidi kufupisha uhai wa Israel
Sep 14, 2023 23:55Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameionya Israel na kusema kuwa, vitisho vya Tel Aviv dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran havitakuwa na matokeo mengine isipokuwa kuendelea kufupisha uhai wa utawala wa Kizayuni.
-
Sisitizo la Iran la kutekelezwa makubaliano ya usalama na Iraq
Sep 14, 2023 10:48Akizungumza tarehe 11 Septemba hapa mjini Tehran na Bafel Talabani, Mkuu wa Muungano wa Kizalendo wa Kurdistan ya Iraq, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya ametaka makubaliano ya usalama yaliyofikiwa kati ya Iran na Iraq yatekelezwe haraka iwezekanavyo.
-
Raisi: Ukraine haijawasilisha ushahidi wa madai ya kutumwa silaha za Iran kwa Russia wakati wa vita
Sep 14, 2023 07:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Waukraine wameshindwa kuwasilisha nyaraka zozote zinazoonyesha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iliipatia silaha Russia wakati wa vita.
-
Ebrahim Raisi: Iran imethibitisha kuwa ni rafiki wa Iraq katika nyakati ngumu
Sep 14, 2023 04:09Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kusita kutoa msaada wowote kwa ajili ya kuihami Iraq katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh (ISIS) na imethibitisha kivitendo kuwa ni rafiki mwaminifu wa Iraq katika nyakati ngumu.
-
Iran yajibu taarifa ya troika ya Ulaya na Marekani dhidi yake katika Bodi ya Magavana wa IAEA
Sep 14, 2023 04:06Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Inasikitisha kuona kwamba Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Marekani ambazo zina malengo na misimamo mahususi dhidi ya Iran zimetumia vibaya ushirikiano wa kiufundi wa Iran na IAEA kama msingi wa ushirikiano wao, kujinufaisha kisiasa madola hayo ya Magharibi."
-
Spika wa Bunge la Iran aelezea masikitiko yake kwa serikali na watu wa Libya baada ya mafuriko
Sep 13, 2023 23:25Katika ujumbe wake kwa Spika mwezake wa Bunge la Libya, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameelezea masikitiko yake kwa serikali na wananchi wa Libya kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
-
Australia yaiwekea Press TV ya Iran vikwazo katika hujuma nyingine dhidi ya uhuru wa kujieleza
Sep 13, 2023 10:25Katika shambulio lingine lililoongozwa na nchi za Magharibi dhidi ya uhuru wa kujieleza nchini Iran, serikali ya Australia imewawekea vikwazo watu kadhaa nchini Iran na pia televisheni maarufu ya Kiingereza ya Iran ijulikanayo kama Press TV.
-
Abdollahian: Kuwapa fursa magaidi ni kwa madhara ya usalama wa eneo
Sep 13, 2023 08:20Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuwapa magaidi hata saa moja ni hatari kwa usalama wa Iraq, Iran, eneo na eneo la Kurdistan la Iraq.
-
Balozi wa Saudi Arabia: Ukurasa mpya umefunguliwa katika uhusiano wa Tehran na Riyadh
Sep 13, 2023 07:49Balozi mpya wa Saudi Arabia nchini Iran ameonyesha kufurahishwa na kufunguliwa ukurasa mpya wa uhusiano baina ya Tehran na Riyadh na kwamba, uhusiano huo utakuwa imara katika nyanja zote.