Abdollahian: Kuwapa fursa magaidi ni kwa madhara ya usalama wa eneo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i102192-abdollahian_kuwapa_fursa_magaidi_ni_kwa_madhara_ya_usalama_wa_eneo
Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuwapa magaidi hata saa moja ni hatari kwa usalama wa Iraq, Iran, eneo na eneo la Kurdistan la Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 13, 2023 08:20 UTC
  • Abdollahian: Kuwapa fursa magaidi ni kwa madhara ya usalama wa eneo

Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuwapa magaidi hata saa moja ni hatari kwa usalama wa Iraq, Iran, eneo na eneo la Kurdistan la Iraq.

Hussein Amir-Abdollahian amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Iraq na kubainisha kwamba, Iran na Iraq zilikuwa na majadiliano muhimu kuhusu utekelezaji kamili wa makubaliano ya usalama kati ya nchi hizo mbili, na Iran ina nia ya dhati ya kudhamiini usalama wake.

Amir Abdollahian ameongeza kuwa, maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Iraq na Fouad Hossein wamechukua hatua nzuri sana hii leo kuhusiana na kuondolewa makundi ya kigaidi katika maeneo ya karibu na mipaka ya Iran, kuhamishiwa katika kina kirefu cha ardhi ya Iraq katika eneo la Kurdistan la Iraq, juhudi za kuwapokonya silaha na katika hatua itakayofuata ni kutekelezwa kikamilifu vipengee vya makubaliano ya usalama yaliyofikiiwa na pande mbili.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, doa jeusi la makundi ya kigaidi ni lazima liondolewe haraka iwezekanavyo katika ukurasa mweupe na wa fahari wa uhusiano wa Iran na Iraq.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Fouad Hossein pia amesema katika mkutano huo wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji wake kwamba, serikali ya Baghdad inafungamana kikamilifu na makubaliano ya usalama na Iran na kwamba, mpango huu utakamilika ifikapo tarehe 15 Septemba.

Fouad Hossein sambamba na kueleza kuwa katiba ya Iraq hairuhusu matumizi ya ardhi ya nchi hii kushambulia nchi nyingine ameeleza kwamba, ushirikiano wa kiusalama kati ya Iraq na Iran kimsingi unatokana na katiba.