-
Spika wa Bunge la Pakistan: Mapambano ya Iran yamekuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine
May 11, 2023 07:47Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan amesema mapambano ya kishujaa ya Iran mbele ya changamoto mbalimbali yamekuwa mfano wa kkuigwa kwa mataifa mengine duniani.
-
Nchi za Ulaya zitadidimia kwa kufuata kibubusa nyayo za Marekani
May 11, 2023 03:08Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran anasema nchi za Ulaya zitatumbukia katika hali mbaya isiyoweza kurekebishwa ikiwa hazitafanikiwa kutupilia mbali minyororo ya kujidhalilisha mbele ya Marekani na kuunga mkono kibubusa sera za Washington.
-
Amir-Abdollahian: Iran itamteua balozi wake Saudi Arabia hivi karibuni
May 11, 2023 02:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian anasema hivi karibuni kwamba Iran itamteua balozi wake huko Saudi Arabia huku nchi hizi mbili zikiwa katika mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida kufuatia makubaliano yaliyofikiwa huko China mwezi Machi uliopita.
-
Wafanyabiashara wa nchi 71 duniani wameshiriki maonyesho ya Iran Expo 2023
May 11, 2023 01:33Mkuu wa Maonyesho ya Kimataifa ya Iran Expo 2023 amesema maooneysho ya mwaka huu yamevutia idadi kubwa ya wafanyabiashara na kuongeza kuwa: "Wafanyabiashara, maafisa wa biashara wa serikali kutoka nchi 71 za dunia wamesafiri hadi Iran kutembelea mambo kadhaa ambayo yamefanywa."
-
Kan'ani amjibu Blinken: Washington ishughulikie ukiukaji wa haki za binadamu ndani ya Marekani, isiingilie mambo ya wengine
May 10, 2023 09:54Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeitaka Marekani kushughulikia ukiukaji wa haki za binadamu unaofanyika nchini humo badala ya kuingilia masuala ya nchi nyingine na kuhukumu kiwango chao cha uhuru wa kujieleza.
-
Meja Jenerali Salami: Matukio makubwa yako njiani yaja na haki itadhihiri tena katika eneo
May 10, 2023 03:26Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametoa kauli kuhusiana na matukio yaliyojiri karibuni katika eneo la Asia Magharibi na kusisitiza kwamba matukio makubwa yako njiani yanakuja na haki itadhihiri tena katika eneo.
-
Vikwazo vya dawa dhidi ya Iran, jinai ya wazi ya Wamagharibi
May 09, 2023 21:53Mkuu wa Jumuiya ya Kuwahami Wagonjwa wa Thalassemia nchini Iran amesema kuwa, wagonjwa 662 wa ugonjwa huo wamefariki dunia humu nchini katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kutokana na kukosa dawa kwa sababu ya vikwazo vya kidhalimu vya nchi za Magharibi dhidi ya wananchi wa Iran.
-
Iran yaendelea kusisitizia uhusiano mzuri na nchi za bara la Afrika
May 09, 2023 00:57Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Burkina Faso wamekutana na kujadiliana njia mbalimbali za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyuga tofauti.
-
Watu wawili wanyongwa nchini Iran kwa hatia ya kukufuru, kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu
May 08, 2023 07:53Wanaume wawili waliokuwa wametiwa hatiani kwa kukufuru, kuidhalilisha Qur’ani Tukufu, na kuutukana Uislamu, Mtume Muhammad (SAW), na matakatifu mengine ya Kiislamu wamenyongwa nchini Iran.
-
Baqeri: Mlingano wa nguvu unahama kutoka Magharibi na unaelekea Mashariki
May 08, 2023 07:22Mkuu wa Majeshi ya Iran amesema kwamba, kuna kila dalili na ushahidi unaoonesha kuwa nguvu za Marekani na washirika wake wa Magharibi zinazidi kufifia na mlingano wa nguvu duniani hivi sasa umo katika kuhama kutoka Magharibi kuelekea Mashariki mwa dunia.