Iran yaendelea kusisitizia uhusiano mzuri na nchi za bara la Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i97158-iran_yaendelea_kusisitizia_uhusiano_mzuri_na_nchi_za_bara_la_afrika
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Burkina Faso wamekutana na kujadiliana njia mbalimbali za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyuga tofauti.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 09, 2023 00:57 UTC
  • Iran yaendelea kusisitizia uhusiano mzuri na nchi za bara la Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Burkina Faso wamekutana na kujadiliana njia mbalimbali za kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyuga tofauti.

Siasa za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa na uhusiano mzuri na nchi za dunia zikiwemo za bara la Afrika. Siasa kuu za Iran ni kukabiliana na ubeberu wa kambi moja na kuhakikisha kila taifa linapewa haki ya kushiriki vilivyo katika masuala ya dunia na uhuru wa kujiamulia lenyewe mambo yake. 

Soko la bara la Afrika nalo ni kubwa na mashirika ya Iran yanaweza kunufaika sana na soko hilo, ndio maana bara la Afrika linapewa kipaumbele maalumu katika siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Bendera za Iran na Burkina Faso

 

 

Ikiwa ni katika kuendeleza siasa hizo za kulipa umuhimu mkubwa bara la Afrika, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian ameonana na Waziri wa Biashara na Ustawi wa Viwanda wa Burkina Faso,  Serge Gnaniodem Poda, hapa mjini Tehran na wamejadiliana masuala muhimu yakiwemo ya kushirikiana zaidi katika sekta ya sanaa za mikono, viwanda vidogo vidogo na vya katikati na kati na kusisitiza kuwa, kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika nyuga mbalimbali, ni miongoni mwa ajenda kuu za Serikali ya 13 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Waziri wa Biashara na Ustawi wa Viwanda wa Burkina Faso yupo katika ziara ya kikazi hapa nchini Iran akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa watu 14 wa nchi yake.