-
Wafuasi wa Imam Mahdi wakusanyika Jamkaran kuonesha imani na tumaini siku ya Nisf Sha’ban
Feb 04, 2026 10:36Maelfu ya waumini na wafuasi wa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake) wamekusanyika katika Msikiti mtukufu wa Jamkaran, mjini Qom, katika siku tukufu za mwezi wa Sha’ban, na kugeuza eneo hilo kuwa ishara yenye nguvu ya imani, mshikamano, na matarajio yenye matumaini kwa mustakabali.
-
Jalali: Madai ya Trump kwamba anawaunga mkono Wairani hayana msingi
Feb 04, 2026 07:25Balozi wa Iran nchini Russia, Kazem Jalali amepuuzilia mbali matamshi ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani Donald Trump akidai kuwa analiunga mkono na kulisaidia taifa la Iran, akisisitiza kuwa madai hayo hayana msingi wowote.
-
Droni ya upelelezi ya Iran yakamilisha kazi yake kwa mafanikio katika maji ya kimataifa
Feb 04, 2026 04:03Droni ya doria na ya intelijinsia ya vikosi vya ulinzi vya Iran imefanikiwa kukamilisha kwa mafanikio operesheni yake katika maji ya kimataifa huku ripoti zikiarifu kuwa askari wa Marekani wameitungua ndege moja isiyo na rubani sawa na hiyo.
-
Iran yazindua miradi mitatu ya kimkakati ya teknolojia ya anga za mbali
Feb 03, 2026 23:56Iran imezindua rasmi mafanikio matatu ya kimkakati ya ndani ya nchi katika sekta za miundombinu ya anga, mawasiliano na picha za satelaiti katika kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Teknolojia ya Anga za Mbali
-
Iran yawaita mabalozi wa Umoja wa Ulaya kulalamikia tuhuma dhidi ya IRGC
Feb 03, 2026 23:55Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imewaita mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya azimio la hivi karibuni la EU linalolenga Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
Kwa nini Marekani inafuatilia sera ya "mazungumzo na vitisho kwa wakati mmoja" dhidi ya Iran?
Feb 03, 2026 07:49Utawala wa Rais Donal Trump wa Marekani umekuwa ukifuatiilia sera ya "mazungumzo na vitisho" kwa wakati mmoja dhidi ya Iran.
-
Rais Pezeshkian aweka masharti ya mazungumzo na Marekani, 'hakuna vitisho, hakuna mashinikizo'
Feb 03, 2026 04:59Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema amemwagiza waziri wa mambo ya nje kuendelea na mazungumzo na Marekani, alimradi yafanyika katika mazingira ya kuheshimiana na yasiyo na vitisho.
-
Shamkhani: Mazungumzo ya Marekani yanaweza kuzaa matunda iwapo tu yataonyesha heshima, mantiki
Feb 03, 2026 04:40Afisa wa ngazi ya juu wa Iran amesema kuwa mazungumzo yajayo ya nyuklia na Marekani yanaweza kuwa na tija iwapo tu yatajiepusha na anga ya vitisho na madai yasiyo na mantiki, na kusisitiza kuwa Tehran haina nia ya kuhamisha nje ya nchi akiba yake ya urani iliyorutubishwa chini ya makubaliano yoyote.
-
Ripoti: Iran, Marekani kufanya mazungumzo ya nyuklia mjini Istanbul
Feb 03, 2026 04:23Iran na Marekani zinapanga kufanya duru mpya ya mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran.
-
'Hakuna Mmarekani atakayesalimika’: Mkuu wa Majeshi ya Iran asema vikosi vya jeshi viko tayari kulipiza kisasi
Feb 03, 2026 00:20Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonya kuwa mahesabu yoyote ghalati ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu yatakabiliwa na jibu kali. Amesema kuwa Iran imejiandaa kikamilifu kwa makabiliano na kulipiza kisasi.