Amir Hatami: Hakuna adui hata mmoja anayepaswa kubakia hai
-
Meja Jenerali Amir Hatami
Kamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameiagiza Makao Makuu ya Operesheni ya Jeshi kufuatilia nyendo na vitendo vya adui kwa jicho la kushuku na usahihi mkubwa, mara kwa mara, na kutekeleza mipango ya kukabiliana na mbinu za mashambulizi ya adui kwa wakati unaofaa.
Katika mawasiliano ya mtandaoni kutoka kwenye mojawapo ya vituo vya Uongozi na Udhibiti vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesema kwamba jeshi liko tayari kukabiliana na uovu wowote wa adui katika nyanja za mashambulizi na ulinzi, na amewahutubia makamanda akisema: Ni muhimu kufuatilia mienendo na vitendo vya maadui kwa jicho la kushuku na usahihi mkubwa, mara kwa mara, na kutekeleza mipango ya kukabiliana na mbinu za adui kwa wakati mwafaka.
Meja Jenerali Hatami amesisitiza kuwa: "Iwapo adui atajaribu kufanya mashambulizi ya nchi kavu, hakuna askari wake hata mmoja anayepaswa kubakia hai."
Akizungumzia harakati maarufu ya wananchi ya "Jitoe Mhanga Maisha Yako kwa Ajili ya Iran" ambayo imeanzishwa sambamba na vitisho vya Marekani na Uzayuni vya kushambulia pwani, visiwa na mipaka ya Iran ya Kiislamu, Meja Jenerali Hatami amesema: Wafanyakazi wote wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wako tayari kusabilia maisha yao kwa ajili ya Iran pendwa" na wamesimama kwa nguvu zao zote na kutoa mhanga maisha yao ili kulinda ardhi na fahari ya Iran ya Kiislamu.