Brigedia Jenerali Fadavi: Ujinga wa Marekani umewaletea matatizo walimwengu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137724-brigedia_jenerali_fadavi_ujinga_wa_marekani_umewaletea_matatizo_walimwengu
Mshauri wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: “Walimwengu sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa ya nishati kutokana na upumbavu wa shetani mkubwa, Marekani.”
(last modified 2026-04-01T04:13:35+00:00 )
Apr 01, 2026 04:13 UTC
  • Brigedia Jenerali Fadavi: Ujinga wa Marekani umewaletea matatizo walimwengu

Mshauri wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: “Walimwengu sasa wanakabiliwa na matatizo makubwa ya nishati kutokana na upumbavu wa shetani mkubwa, Marekani.”

Akizungumza karibuni katika mahojiano ya televisheni, Ali Fadavi, Mshauri wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, ameashiria makosa ya kimahesabu ya Marekani na kusema: Kinyume na walivyodhani Wamarekani kwamba wangeweza kuiangamiza Iran, sasa wanataka kufikia malengo madogo na mepesi kabisa.

Akieleza kuwa upumbavu wa Marekani umewanyima watu wa dunia manufaa yao ameongeza kuwa: "Ili kufikia malengo yake katika uvamizi dhidi ya Iran, Marekani imechukua hatua zinazokiuka sheria za kimataifa ambazo nchi zote zinatilia mkazo utekelezaji wake katika vita, na kutambua ukiukaji wake kuwa jinai za kivita." Akizungumzia mashambulizi dhidi ya vituo vya kiraia vya Iran, Brigedia Jenerali Fadavi ameasheria hatua ya kijinai za Marekani na Israel za kushambulia taasisi na maeneo ya kiraia nchini Iran na kusema: "Wakati Marekani imeshindwa kufikia malengo yake, kulenga vituo vya kiraia vya Iran sio tu kumeibua matatizo zaidi, bali pia kumeacha nyuma historia mbaya kwa nchi hiyo, ya kuendelea kukiuka hadharani sheria za kimataifa."