-
Ubunifu wa Iran kwa ajili ya mshikamano, amani na ustawi wa kudumu katika ulimwengu wa Kiislamu
Jan 31, 2023 06:32Muhammad Baqir Qalibaf, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jumatatu ya jana tarehe 30 Januari alisema katika mkutano wa 17 wa Muungano wa Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) uliofanyika nchini Algeria kwamba, ulimwengu wa Kiislamu haujawa na mchango na nafasi inayotakiwa ikilinganishwa na suhula ulizonazo.
-
Iran: Hatubabaishwi na bwabwaja na matamshi ya vitisho ya Marekani
Jan 30, 2023 23:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekosoa porojo na matamshi ya vitisho ya Marekani na kuonya kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itatoa jibu kali kwa hatua yoyote ya uvamizi dhidi ya taifa hili.
-
Shambulio 'butu' lililogonga mwamba dhidi ya kituo cha kijeshi cha Esfahan
Jan 30, 2023 04:53Wizara ya Ulinzi ya Iran ilitangaza usiku wa kuamkia jana Jumapili kuwa, jengo moja la karakana za Wizara ya Ulinzi mjini Esfahan lililengwa na shambulio lililofeli la ndege tatu ndogo zisizo na rubani aina ya Micro Air Vehicle (MAV), ambapo moja ya droni hizo ilitunguliwa, nyingine ilinaswa kwenye mtego wa mitambo ya ulinzi wa anga na droni tatu iliangukia kwenye paa la karakana hiyo na kuripuka.
-
Amir-Abdollahian: Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar ametuletea ujumbe wa upande wa pili wa mazungumzo ya nyuklia
Jan 30, 2023 03:28Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameishukuru Qatar kwa juhudi zake za kuhakikisha mazungumzo ya kuondolewa vikwazo Iran yanazaa matunda na amesema, leo tumepokea ujumbe mbalimbali wa upande wa pili za mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Matarajio ya Iran ya kupata maendeleo ni angavu zaidi kuliko utabiri wa sasa
Jan 30, 2023 10:08Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika kikao chake na mamia ya wazalishaji, wajasiriamali na wanaharakati katika nyuga zinazoegemea elimu kuwa, mustakbali wa taifa na matarajio ya maendeleo ya Iran ni angavu zaidi kuliko utabiri wa hivi sasa.
-
Iran ni ya pili katika nchi za Kiislamu kwenye orodha ya nchi zenye vyuo vikuu vingi
Jan 29, 2023 23:40Katika orodha ya Daraja za Vyuo Vikuu Duniani (ISC World University Rankings) Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshika nafasi ya pili katika nchi za Kiislamu zenye vyuo vikuu vingi, ikiwa na vyuo vikuu 63 ikitanguliwa na Uturuki.
-
Spika wa Bunge la Algeria: Tunataka kuimarisha uhusiano na Iran
Jan 29, 2023 09:52Spika wa Bunge la Algeria amesema: Tunajivunia mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyuga mbalimbali na tunataka kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yetu mawili.
-
Iran yazima mashambulio ya droni katika mkoa wa Isfahan
Jan 29, 2023 09:13Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu vimefanikiwa kuzima mashambulio ya ndege zisizo na rubani (drone) dhidi ya kituo cha kijeshi katika mji wa Isfahan, katikati mwa nchi.
-
Qalibaf: Afrika ni mojawapo ya fursa muhimu za kiuchumi kwa Ulimwengu wa Kiislamu
Jan 29, 2023 04:05Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kabla ya kuondoka Tehran kuelekea ziarani nchini Algeria kwa lengo la kushiriki katika mkutano wa mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuwa: Afrika katika mazingira ya sasa ni moja ya fursa muhimu za kiuchumi na kiutamaduni kwa Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Kadkhodaei: Operesheni ya kumsaka Pompeo na Trump itaendelea hadi haki ipatikane
Jan 28, 2023 23:07Mjumbe wa Baraza la Walinzi wa Katiba nchini Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba mchakato wa kuwafuatilia rais na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani unaendelea kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya maafisa wa Iran na Iraq.