Iran: Hatubabaishwi na bwabwaja na matamshi ya vitisho ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i93496-iran_hatubabaishwi_na_bwabwaja_na_matamshi_ya_vitisho_ya_marekani
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekosoa porojo na matamshi ya vitisho ya Marekani na kuonya kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itatoa jibu kali kwa hatua yoyote ya uvamizi dhidi ya taifa hili.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Jan 30, 2023 23:24 UTC
  • Iran: Hatubabaishwi na bwabwaja na matamshi ya vitisho ya Marekani

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekosoa porojo na matamshi ya vitisho ya Marekani na kuonya kuwa, Jamhuri ya Kiislamu itatoa jibu kali kwa hatua yoyote ya uvamizi dhidi ya taifa hili.

Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, "Marekani inapaswa kutambua wajibu wa kisheria na kimataifa, na matokeo mabaya ya matamshi yake ya vitisho dhidi ya Iran; na inapasa kufikiria mara mbili juu ya matokeo mabaya ya kisiasa ya taarifa za vitisho (dhidi ya Iran)."

Kan'ani amesema hayo kujibu matamshi ya vitisho na propaganda yaliyotolewa hivi karibuni na Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani katika mahojiano na shirika la habari la Al Arabiya la Saudia.

Blinken alibwabwaja kwa kusema, luteka za kijeshi za Marekani na Israel na nchi nyingine waitifaki katika Ghuba ya Uajemi eti zinakusudia kuzima harakati za Iran katika eneo la Asia Magharibi.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani aidha alidai kuwa, eti Iran ilijipotezea fursa yenyewe ya kurejea katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA katika msimu uliopita wa joto, bila kuashiria ukweli kwamba, aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump ndiye aliyeiondoa Washington kwenye mapatano hayo ya kimataifa ya mwaka 2015.

Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Hii ni katika hali ambayo, Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran juzi aliishukuru Qatar kwa juhudi zake za kuhakikisha mazungumzo ya kuondolewa vikwazo Iran na kueleza kuwa, Tehran imepokea ujumbe mbalimbali wa upande wa pili wa mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje  ya Iran amebainisha kuwa, "Serikali ya Marekani inafahamu fika kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe hairuhusu uvamizi au uporaji wowote wa ardhi yake au maslahi yake, na itatoa jibu kali la kujitisha kwa wavamizi."