Jan 30, 2023 03:10 UTC
  • Iran ni ya pili katika nchi za Kiislamu kwenye orodha ya nchi zenye vyuo vikuu vingi

Katika orodha ya Daraja za Vyuo Vikuu Duniani (ISC World University Rankings) Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeshika nafasi ya pili katika nchi za Kiislamu zenye vyuo vikuu vingi, ikiwa na vyuo vikuu 63 ikitanguliwa na Uturuki.

Katika orodha ya mwaka 2022 ya vyuo vikuu duniani iliyochapishwa na ISC, Iran imeshika nafasi ya pili katika nchi za Kiislamu kwa kuwa na vyuo vikuu 63, baada ya Uturuki.
Aidha, kwa upande wa ubora wa vyuo vikuu duniani, Iran imeshika nafasi ya tatu katika nchi za Kiislamu, ikitanguliwa na Saudi Arabia na Misri.
Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, taasisi ya Daraja za Vyuo Vikuu Duniani ya nchi za Kiislamu ni moja ya mifumo ya uainishaji viwango na daraja za vyuo vikuu iliyoasisiwa na kuanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza mwaka 2018 baada ya kufanya tathmini kwa kuzingatia tajiriba ya miaka 10 ya kupima viwango vya vyuo vikuu katika ngazi ya kitaifa na kwa lengo la kutathmini viwango vya vyuo vikuu vya nchi mojamoja na nchi za Kiislamu katika upeo wa kimataifa.
Katika orodha ya kimataifa ya ISC kwa mwaka 2022, kuna jumla ya vyuo vikuu 2,422 kutoka nchi 111 na mabara sita duniani ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina vyuo vikuu 63.../