-
Marandi: Makubaliano ya Marekani na Iran ni hatua erevu ya kuzuia mgogoro wa nishati
Jul 17, 2022 07:21Mohammad Marandi, mchambuzi mwandamizi wa masuala ya kisiasa na mitaala kuhusu Marekani amesema makubaliano kati ya Marekani na Iran ni hatua erevu ambayo kama itachukuliwa itazuia kutokea mgogoro wa nishati katika nchi za Magharibi.
-
Iran karibuni itakuwa kitovu cha kurushia satalaiti katika eneo
Jul 17, 2022 03:37Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imekuwa nguzo ya kurushia satalaiti katika eneo.
-
Kan’ani: Matamshi ya Biden kuhusu Iran yanalenga kuendeleza fitina za Washington
Jul 17, 2022 03:33Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema baadhi ya madai na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakati wa safari ya Rais Joe Biden wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi, ikiwa ni pamoja na matamshi yake akiwa Jeddah si za kweli na hazina msingi wowote.
-
Iran yawawekea vikwazo Wamarekani wanaounga mkono magaidi wa MKO
Jul 16, 2022 23:05Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza orodha mpya ya maafisa wa sasa na wa zamani wa serikali ya Marekani ambao kwa makusudi wamekuwa wakiunga mkono kundi la kigaidi la MKO lililo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran yakanusha madai ya Marekani kuwa imeipa Russia droni za kivita
Jul 16, 2022 07:19Iran imesema Marekani inafuatilia "malengo mahususi ya kisiasa" kwa kudai kwamba Tehran inapanga kuikabidhi Russia mamia ya droni au ndege zisizo na rubani zenye uwezo wa kusheheni silaha za kivita.
-
Jen. Shekarchi: Marekani, Israel zinajua vyema gharama ya kuitishia Iran
Jul 15, 2022 22:14Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zinatambua vizuri kile ambacho kitawafika iwapo zitathubutu kutelekeza kivitendo vitisho vyao dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Amir Abdollahian: Iran itaendeleza juhudi zake katika njia ya kuondoa vikwazo kwa nguvu na mantiki
Jul 15, 2022 07:01Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeazimia ipasavyo katika njia ya maendeleo endelevu ya kiuchumi na kuondolewa vikwazo ilivyowekewa.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Ghadir ni suala la kipekee katika historia ya mwanaadamu
Jul 15, 2022 06:59Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema: Suala la Ghadir ni kadhia ya kipekee katika historia ya mwanaadamu, na Mwenyezi Mungu hajalipa tukio lolote lile umuhimu mkubwa kuliko tukio la Ghadir Khum.
-
Iran yalamikia rasmi hatua ya Uswidi ya kumfunga Muirani kwa tuhuma bandia
Jul 15, 2022 02:41Iran imemuita balozi mdogo wa Uswidi mjini Tehran na kumkabidhi malalamiko ya kupinga hukumu ya mahakama ya Uswidi dhidi ya raia wa Iran ambaye amefungwa kifungo cha maisha jela kutokana na tuhuma zisizo na msingi zilizotolewa dhidi yake na kundi la kigaidi la MKO linaloipinga Iran.
-
Tamko la Iran kufuatia taarifa ya Biden na Lapid
Jul 15, 2022 02:34Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa tamko kufuatia taarifa ya pamoja ya Rais Joe Biden wa Marekani na waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Yair Lapid na kusema : "Maadamu utawala bandia wa Israel ni kituo cha kwanza cha safari za marais wa Marekani na lengo lao kuu ni kulinda usalama wa utawala huo, mataifa ya eneo hayatashuhudia amani, uthabiti na utulivu."