Tamko la Iran kufuatia taarifa ya Biden na Lapid
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i85890-tamko_la_iran_kufuatia_taarifa_ya_biden_na_lapid
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa tamko kufuatia taarifa ya pamoja ya Rais Joe Biden wa Marekani na waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Yair Lapid na kusema : "Maadamu utawala bandia wa Israel ni kituo cha kwanza cha safari za marais wa Marekani na lengo lao kuu ni kulinda usalama wa utawala huo, mataifa ya eneo hayatashuhudia amani, uthabiti na utulivu."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 15, 2022 02:34 UTC
  • Tamko la Iran kufuatia taarifa ya  Biden na Lapid

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa tamko kufuatia taarifa ya pamoja ya Rais Joe Biden wa Marekani na waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel Yair Lapid na kusema : "Maadamu utawala bandia wa Israel ni kituo cha kwanza cha safari za marais wa Marekani na lengo lao kuu ni kulinda usalama wa utawala huo, mataifa ya eneo hayatashuhudia amani, uthabiti na utulivu."

Sambamba na mkutano wa pamoja na waandishi habari katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na Israel, Biden na Lapid walitia saini taarifa ya pamoja.

Katika taarifa hiyo, Marekani imeahidi kuchukua hatua za kuibua muundo katika eneo la Asia Magharibi ambao utaimarisha zaidi uhusiano wa utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi za eneo na kueneza mchakato huo ili kujumuisha nchi zaidi za Kiislamu.

Kufuatia taarifa hiyo, Nasser Kan’ani Chafi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe katika Twitter na kuandika: "Taarifa ya pamoja ya  Biden na Lapid imesisitiza kuhusu 'ahadi imara ya Marekani ya kulinda usalama wa Israel na kuhakikisha kuwa Israel inakuwa na nguvu zaidi za kijeshi katika eneo. Isifahimike kimakosa, lengo lao si Iran tu bali wanataka nchi za Kiarabu na Kiislamu zitambue kuwa utawala wa Kizayuni ndio wenye nguvu zaidi. Kwa hivyo sasa iko wazi kuhusu chanzo kikuu cha tishio kwa eneo.

Nasser Kan’ani Chafi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Kan'ani aidha amesema: "Maadamu utawala bandia wa Israel ni kituo cha kwanza cha safari za marais wa Marekani na lengo lao kuu ni kulinda usalama na utawala huo, mataifa ya eneo hayatashuhudia amani, uthabiti wala utulivu. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kuwa usalama wa majirani zake ni usalama wake."

Joe Biden, Rais wa Marekani Jumatano aliwasili katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ambazo zimepachikwa jina la Israel kwa lengo la kufanya mazungumzo na wakuu wa utawala wa Kizayuni na kisha aelekee Saudi Arabia.