-
Rais wa Iran: Kuna haja ya kuweko mshikamano baina ya mataifa ya Kiislamu ili kukabiliana na Israel
Mar 01, 2022 04:45Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uadui wa mabeberu dhidi ya mataifa ya eneo la Asia Magharibi haujapungua na kusisitiza kwamba, kuna haja na udharura kwa nchi za Kiislamu na Waislamu kuwa na mshikamano ili kukabiliana na hatua za utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel.
-
Khatibzadeh: Hatuko Vienna kwa ajili ya kufikia makubaliano mapya
Feb 28, 2022 10:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema kuwa, ushiriki wa ujumbe wa Iran katika mazungumzo ya Vienna si kwa ajili ya kufikia makubaliano mapya na kueleza kuwa, hali ya hivi sasa si ya utata kwa Washington na Ulaya, na kwamba Jamhuri ya Kiislamu haitavuka mistari yake myekundu.
-
Safari ya Kamanda wa Jeshi la Anga la Iran nchini Pakistan na diplomasia ya Tehran ya ulinzi amilifu
Feb 28, 2022 07:39Jumapili ya jana tarehe 27 Februari, Brigedia Jenerali Hamid Vahedi, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasili katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad kwa minajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na maafisa wa kijeshi na kisiasa wa nchi hiyo.
-
Shamkhani: Kuweko wanajeshi wa Marekani ndicho kikwazo cha kupatikana amani Syria
Feb 27, 2022 22:53Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, uwepo wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Syria ndicho kikwazo kikuu cha kupatikana amani katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Kuongezeka kwa kasi biashara ya nje ya Iran katika serikali ya 13 licha ya kuwepo vikwazo vya upande mmoja vya Marekani
Feb 27, 2022 22:51Biashara ya nje ya Iran katika kipindi cha miezi 11 iliyopita imefikia kiwango cha dola bilioni 90, ambalo ni ongezeko la asilimia 38 ikilinganishwa na muda kama huo katika mwaka uliopita.
-
Wanafunzi 20 wa shule za Ulimwengu wa Kiislamu wafanikiwa kuingia fainali za mashindano ya Qur'ani Tukufu
Feb 26, 2022 09:06Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Qur'ani, Itra na Sala cha Wizara ya Elimu na Malezi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, vijana wadogo 20 wameingia kwenye fainali ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa wanafunzi wa shule za Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Ravanchi: Utawala wa Syria haupaswi kudhoofishwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi
Feb 26, 2022 04:17Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, kuwepo kinyume cha sheria majeshi ya kigeni katika baadhi ya maeneo ya Syria kumetayarisha mazingira ya harakati na shughuli za makundi ya kigaidi nchini Syria.
-
Iran kuendelea kurutubisha urani kwa 20% hata ikiondolewa vikwazo
Feb 25, 2022 23:09Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema Jamhuri ya Kiislamu itaendelea kuzalisha madini ya urani iliyoritubishwa kwa kiwango cha asilimia 20, hata kama itaondolewa vikwazo katika mazungumzo ya Vienna yanayolenga kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Mauzo ya mafuta ya Iran nje ya nchi yaongezeka kwa 40%
Feb 25, 2022 23:08Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema uuzaji wa mafuta yake katika soko la kimataifa umeongezeka kwa asilimia 40 katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, licha ya vikwazo dhidi ya taifa hili.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Hatua za kichochezi za NATO zimeifanya hali katika eneo iwe tata
Feb 25, 2022 09:39Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehrah amesema, hatua za kichochezi zilizochukuliwa na shirika la kijeshi la NATO kwa uongozi wa Marekani zimetatanisha hali ya mambo katika eneo; na si hasha zikaifanya iwe tata zaidi.