-
Rais Raisi: Uhusiano wa kiuchumi na nchi jirani unazidi kuboreka
Jan 09, 2022 04:41Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, uhusiano wa kiuchumi baina ya Iran na nchi zingine za kieneo umeboreka.
-
Kiongozi Muadhamu: Wairani wamegeuza kuuawa shahidi Jenerali Soleimani kuwa ni fursa
Jan 09, 2022 04:38Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema maadui walidhani kuuawa shahidi kamanda shujaa katika vita dhidi ya ugaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimaini kungekuwa tishio kwa Iran lakini watu wa Iran wamegeuza tukio hilo kuwa fursa kutokana na imani yao ya kidini.
-
Iran: Mazungumzo mazuri yanawezekana iwapo Wamagharibi wataonyesha nia njema
Jan 09, 2022 01:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema kufikia mapatano mazuri ni jambo linalowezekana katika mazungumzo yanayonedelea Vienna kuhusu kuondolewa Iran vikwazo lakini akasisitiza kuwa, hilo litawezekana iwapo upande wa Magharibi utaonyesha nia njema.
-
Iran yaijia juu WSJ ya US kwa kuchapisha makala ya kipumbavu
Jan 08, 2022 09:10Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelikosoa vikali gazeti la Kimarekani la Wall Street Journal kwa kuchapisha makala ya kipumbavu na ya kihasama dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, wakati huu wa kuendelea kufanyika mazungumzo ya kuiondolea vikwazo Iran huko Vienna.
-
Instagram yafuta jumbe zinazozungumzia Jenerali Soleimani
Jan 08, 2022 09:02Wananchi wa Iran wameanzisha kampeni ya kulalamikia hatua ya mtandao wa kijamii wa Instagram ya kuendelea kufuta jumbe zinazohusiana na Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Mwenendo chanya wa mazungumzo ya Vienna; kilichobakia ni azma ya kweli ya Wamagharibi
Jan 08, 2022 06:39Mazungumzo kati ya wawakilishi wa Iran na wa kundi la 4+1 linaloundwa na Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuhusu kuiondolea Iran vikwazo yangali yanaendelea huku vikao mbalimbali nyeti na muhimu kuhusu masuala tofauti vikifanyika mtawalia na kwa wakati mmoja.
-
Ayatullah Seddiqi: Wanafunzi wa Shahidi Soleimani watang'oa mizizi ya ubeberu Asia Magharibi.
Jan 07, 2022 09:49Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa: Kambi iliyoasisiwa na shujaa Shahidi Qasem Soleimani katika vita vikali dhidi ya batili itawaangamiza kabisa Wamarekani na mamluki wao katika eneo hili la Magharibi mwa Asia.
-
Iran: Kutimuliwa Marekani Asia Magharibi ni jibu kwa ujuha na uhayawani wa adui wa kumuua Qassem Soleimani
Jan 07, 2022 04:38Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu imetangaza kuwa, kutimuliwa utawala wa Marekani katika eneo nyeti la Asia Magharibi ni jibu kwa ujuha na ujinga wa adui katika kumuua Luteni Jenerali Qassem Soleimani.
-
Iran: Korea Kusini lazima itulipe deni letu
Jan 07, 2022 00:04Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa na kiongozi wa ujumbe wa Iran katika mazungumzo ya Vienna amesema Korea Kusini haina chaguo jingine isipokuwa kutekeleza wajibu wake na kuilipa Jamhuri ya Kiislamu deni lake.
-
Iran: Wakazakhstan wanaweza kutatua matatizo yao bila uingiliaji wa maajinabi
Jan 07, 2022 00:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema wananchi wa Kazakhstan wana uwezo wa kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, pasi na kutegemea uingiliaji wa madola ajinabi.