Rais Raisi: Uhusiano wa kiuchumi na nchi jirani unazidi kuboreka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78996-rais_raisi_uhusiano_wa_kiuchumi_na_nchi_jirani_unazidi_kuboreka
Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, uhusiano wa kiuchumi baina ya Iran na nchi zingine za kieneo umeboreka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 09, 2022 04:41 UTC
  • Rais Raisi: Uhusiano wa kiuchumi na nchi jirani unazidi kuboreka

Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, uhusiano wa kiuchumi baina ya Iran na nchi zingine za kieneo umeboreka.

Rais ameyasema hayo leo asubuhi katika kikao cha  Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, na kuongeza kuwa, uhusiano wa kiuchumi baina ya Iran na nchi za eneo umeimarika mara tatu zaidi katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Aidha amesema, ahadi zilizotolewa na serikali yake kuhusu mlingano katika sera za kigeni zinaendelea kutekelezwa.

Raisi aidha amesema kusambaratisha vikwazo ni moja kati ya masuala muhimu ambayo serikali inafuatilia na suala la pili ni kuondolewa vikwazo.

Spika wa Bunge la Iran Mohammad Baqer Qalibaf

Rais wa Iran aidha amesema serikali yake pia inafuatilia kwa karibu suala la kuhakikisha kuwa wananchi wana imani na serikali.

Kadhalika amesema leo kuwepo ushirikiano wa karibu baina ya bunge na serikali ni jambo la dharura.

Seyyid Ebrahim Raisi ameongeza kuwa, lengo jingine la serikali ni kuhakikisha uchumi wa nchi unastawi kwa kiwango cha asilimia nane kwa mwaka.