-
Wairani washiriki maziko ya mashahidi wao 250, Kiongozi Muadhamu atuma ujumbe
Jan 06, 2022 10:04Wananchi wa Iran wamejitokeza kwa wingi katika maziko ya mashahidi wao 250 waliouawa wakati wa vita vya miaka minane vya kujihami kutakatifu vilivyoanzishwa na utawala wa kidikteta wa Saddam wa Iraq dhidi ya dola changa wakati huo la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Spika Qalibof: Mashahidi ni historia ya uhuru na kukomboka
Jan 06, 2022 04:51Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: mashahidi ni historia nzima ya kuwa huru na kukomboka.
-
Mahakama ya Iran yakosoa sera za kupenda vita za Wamagharibi
Jan 05, 2022 23:20Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amekosoa vikali sera za kupenda na kuchochea vita za nchi za Magharibi, huku akizilaani nchi hizo kwa madai yao bandia kuhusu suala la haki za binadamu.
-
Uzayuni hauna nafasi yoyote katika mustakbali wa dunia
Jan 05, 2022 23:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu upayukaji wa waziri wa mambo ya nje wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusisitiza kuwa, Tehran iko imara katika kulinda maslahi yake ya kitaifa na kwamba, Uzayuni hauna nafasi katika mustakbali wa dunia.
-
Brigedia Jenerali Qaani: Wauaji wa Kamanda Soleimani hawatakuwa salama
Jan 05, 2022 04:15Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Wauaji wa Luteni Jenerali Qasem Soleimani walidhani kuwa wameshinda kwa kumuua, lakini hawakujua kwamba hawatakuwa salama.
-
Sheikh Naim Qassem: Kamanda Soleimani ni shahidi wa Umma
Jan 05, 2022 04:15Akizungumzia mafanikio ya Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Kamanda Soleimani alikuwa shahidi wa Umma.
-
Uzalishaji wa kifaa cha kwanza cha kugundua corona cha omicron nchini Iran
Jan 05, 2022 04:14Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Kashan mkoa wa Isfahan nchini Iran ametangaza mafanikio ya utengenezaji wa kifaa cha kwanza cha Kiirani cha kutambua kirusi cha corona aina ya omicroni.
-
China: Marekani ilitenda jinai ya kivita kwa kumuua Qasem Soleimani
Jan 04, 2022 23:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema Marekanin ilitenda jinai ya kivita kwa kumuua Luteni Jenerali Qasem Soleimani, kamanda wa Iran aliyeongoza vita dhidi ya ugaidi.
-
Meja Jenerali Bagheri: Sifa za kiroho za shahidi Soleimani ni somo kubwa kwa vizazi vijavyo
Jan 04, 2022 10:11Kamanda Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Iran amesema, kila moja ya sifa za kiroho, hali na kumbukumbu za shahidi Qasem Soleimani zitakuwa somo kubwa kwa watu wote wa Iran, eneo, vijana na vizazi vijavyo.
-
Luteni Jenerali shahidi “Qassem Soleimani” nembo ya matumaini, kujiamini, ushujaa na siri ya muqawama na ushindi
Jan 04, 2022 09:29Jumatatu ya jana tarehe 3 Januari 2022, ilisadifiana na kumbukumbu ya mwaka wa pili wa mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyofanywa na serikali ya Marekani.