Spika Qalibof: Mashahidi ni historia ya uhuru na kukomboka
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78888-spika_qalibof_mashahidi_ni_historia_ya_uhuru_na_kukomboka
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: mashahidi ni historia nzima ya kuwa huru na kukomboka.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 06, 2022 04:51 UTC
  • Spika Qalibof: Mashahidi ni historia ya uhuru na kukomboka

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema: mashahidi ni historia nzima ya kuwa huru na kukomboka.

Mohammad Baqer Qalibaf amesema hayo leo katika shughuli ya kusindikiza viwiliwili vya mashahidi wa vita vya Kujihami Kutakatifu iliyofanyika mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo sambamba na kutoa salamu za rambirambi na mkono wa pole kwa mnasaba wa siku aliyokufa shahidi Bibi Fatimatu-Zahra (AS) na kuenzi kumbukumbu ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wa Vita vya Kulazimishwa na mashahidi Walinzi wa Haram amesisitizia kuendelezwa njia ya mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Spika wa Bunge la Iran ameongeza kuwa, kipindi cha sasa ni hasasi na cha kupata ibra na mazingatio makubwa na yasiyo na kifani viongozi walioko madarakani ili watambue kuwa mashahidi wapendwa na wenye thamani kubwa walijitokeza katika medani kwa ikhlasi na kuzitoa mhanga roho zao kwa ajili ya Uislamu, Mapinduzi na Iran ya Kiislamu.

Shughuli ya kuvisindikiza viwiliwili vya mashahidi 250 wa zama za Vita vya Kujihami Kutakatifu imefanyika leo kote nchini katika Iran ya Kiislamu sambamba na kumbukumbu ya siku aliyokufa shahidi Bibi Fatimatu-Zahra (SA).../