-
Hamad bin Jassim: Maafikiano tarajiwa ya madola Magharibi na Iran ni fursa ya kupunguza mizozo
Dec 30, 2021 04:46Waziri Mkuu wa zamani wa Qatar amezungumzia mwenendo wa mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 4+1 yanayoendelea huko Vienna Austria na kueleza kwamba, maafikiano tarajiwa baina ya madola Magharibi na Iran ni fursa ya kupunguza mizozo katika eneo la Asia Magharibi.
-
Mfalme wa Saudia atoa bwabwaja mpya dhidi ya Iran na muqawama
Dec 30, 2021 01:09Mfalme wa Saudi Arabia ameituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, eti inavuruga usalama na kuhatarisha amani ya eneo la Asia Magharibi.
-
Global Times: Maendeleo ya nyuklia ya Iran ni ushahidi wa kumalizika ubabe wa Marekani
Dec 30, 2021 00:07Gazeti la Global Times limeandika kuwa, kadhia ya nyuklia ya Iran na hali ya sasa katika mazungumzo ya Vienna inaashiria hali ngumu ya Marekani, na hali hiyo ni kielelezo kuwa "zama za kuhodhi na ubabe wa dola ya Marekani zimekwisha."
-
Iran yalaani jinai za utawala wa Kizayuni za kushambuia maghala ya chakula nchini Syria
Dec 29, 2021 08:26Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulio ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni katika ardhi ya Syria hususan jinai zake za kushambulia maghala ya vyakula na madawa katika bandari ya Ladhakia.
-
Rais wa Iran kuitembelea Russia kufuatia mwaliko wa Putin
Dec 29, 2021 04:17Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anatazamiwa kuitembelea Russia mapema mwaka ujao 2022, kufuatia mwaliko wa mwenzake wa nchi hiyo, Vladimir Putin.
-
Iran: Inawezekana kufikia makubaliano mazuri katika mazungumzo ya Vienna
Dec 29, 2021 01:07Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza matumaini yake ya kufikiwa mapatano ya kuridhisha katika mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 4+1 linaloundwa na mataifa ya Russia, China, Uingereza, Ufaransa pamoja Ujerumani yanayoendelea huko Vienna, Austria.
-
Kamanda: Adui hawezi kustahamili gharama za makabiliano na Iran
Dec 29, 2021 01:02Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amewashauri maadui wasithubutu kupima uwezo wa kijeshi wa Iran kwa kufanya chokochoko kwani hawataweza kustahamili gharama za vita vya pande zote na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kuondolewa vikwazo Iran; siri ya mafanikio ya mazungumzo ya Vienna
Dec 28, 2021 08:56Mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 4+1 linaloundwa na mataifa ya Russia, China, Uingereza, Ufaransa pamoja Ujerumani yaliendelea tena leo huko Vienna Austria maudhui kuu ikiwa ni suala la kuondolewa vikwazo na kutilia mkazo mapendekezo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu masuala mawili muhimu, yaani uhakika kwamba vikwazo vimeondolewa na dhamana yake.
-
Jenerali wa Marekani akiri, Iran ina uwezo mkubwa wa makombora
Dec 28, 2021 06:20Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) amekiri kuwa Iran ina uwezo mkubwa wa makombora na kusisitiza kwamba makombora ya Iran yanaweza kupiga eneo lolote wanalotaka kwa umakini na kiwango kikubwa.
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Waislamu: Umoja ndiyo silaha ya kupambana na maadui wa Umma
Dec 28, 2021 06:10Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, umoja na mshikamano wa Waislamu ndiyo silaha pekee inayoweza kutumiwa kwa ajili ya kupambana na njama zinazofanywa dhidi ya Uislamu.