Kamanda: Adui hawezi kustahamili gharama za makabiliano na Iran
(last modified 2021-12-29T04:32:40+00:00 )
Dec 29, 2021 04:32 UTC
  • Kamanda: Adui hawezi kustahamili gharama za makabiliano na Iran

Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amewashauri maadui wasithubutu kupima uwezo wa kijeshi wa Iran kwa kufanya chokochoko kwani hawataweza kustahamili gharama za vita vya pande zote na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Meja Jenerali Gholam Ali Rashid, Kamanda wa Divisheni Kuu ya Khatam al-Anbiya (SAW) Majeshi ya Iran amesema: "Tishio lolote kwa vituo vya nyuklia na jeshi la Iran litakabiliwa na jibu kali."

Aidha amesema maadui wanapaswa kufahamu kuwa, daima tunawatazama na tuko tayari na tutahakikisha wanapata gharama na hasara kubwa kuliko yale faida yoyote watakayopata katika chokockokko zao.

Kamanda huyo amesema kuamini nguvu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutmsaidia adui kutopata hasara kubwa.

Matamshi hayo yamekuja kufuatia kuongozeka taharuki baina ya Iran kwa upande mmoja, na Marekani na waitifaki wake, hasa utawala wa Israel, kwa upande wa pili.  Taharuki hizo zimeibuliwa hasa wakati huu wa kufanyika mazungumzo ya Vienna ya kuondolewa Iran vikwazo.

Mazungumzo ya Vienna ya kuondolewa Iran vikwazo

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeashiria kuwa utaishambulia Iran. Waziri wa Vita wa Israel Benny Gantz amenukuliwa akiwaambia maafisa wa Marekani kuwa ameamuru jeshi la utawala huo litayarisha mpango wa kushamabulia kijeshi vituo vya nyuklia vya Iran.

Makamanda wa kijeshi Iran wameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel utapata jibu kali ukijaribu kuanzisha hujuma yoyote ile.

 

Tags