Mfalme wa Saudia atoa bwabwaja mpya dhidi ya Iran na muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i78612-mfalme_wa_saudia_atoa_bwabwaja_mpya_dhidi_ya_iran_na_muqawama
Mfalme wa Saudi Arabia ameituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, eti inavuruga usalama na kuhatarisha amani ya eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Dec 30, 2021 01:09 UTC
  • Mfalme wa Saudia atoa bwabwaja mpya dhidi ya Iran na muqawama

Mfalme wa Saudi Arabia ameituhumu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwamba, eti inavuruga usalama na kuhatarisha amani ya eneo la Asia Magharibi.

Mfalme Salman bin Abdul-Aziz Aal Saud ameendelea na bwabwaja zake kwa kusema kuwa, mhimili wa muqawama katika eneo la Asia Magharibi ikiwemo Lebanon na Yemen ndio unaosababisha migogoro katika mataifa haya na akauvua utawala wake na kuhusika kwa namna yoyote katika migogoro hii.

Mfalme wa Saudia ambaye nchi yake imetenda jinai za kutisha huko nchini Yemen amesema hayo usiku wa kumkia leo katika hotuba yake katika Baraza la Shura la Saudia aliyoitoa kwa njia ya mawasiliano ya intaneti ambapo ametoa madai yasiyo na msingi kabisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 

Amesema, Iran ni nchi jirani, tuna matumaini kwamba, itabadilisha mwenendo wake hasi na kuelekea upande wa mazungumzo na ushirikiano.

Kadhalika Mfalme wa Saudia amedai kwamba, Iran haitoi ushirikiano kwa jamii ya kimataifa kuhusiana na miradi yake ya nyuklia pamoja na mpango wake wa kupanua mfumo wa makombora ya balistiki.

Mfalme wa Saudia ametoa madai hayo katika hali ambayo, walimwengu wanaendelea kushuhudia mauaji ya kutisha dhidi ya wanawake na watoto wadogo nchini Yemen kufuatia vita dhidi ya nchi hiyo vinavyoendesha na Saudia na washirika wake.

Ripoti mbalimbali zimebainisha na kuweka wazi jinai na mauaji ya kutisha yaliyofanywa na Saudia na washirika wake huko nchini Yemen huku utawala huo ukipewa jinai za muuaji wa watoto.