-
Iran yalaani vitisho vya kijeshi vya wazi vya Trump; yalitaka Baraza la Usalama kuchukua hatua
Dec 31, 2025 23:13Iran imelaani rasmi vitisho "vikubwa na vya wazi" vya vita vya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu uwezo wa kiulinzi na miraidi ya nyuklia ya nchi hii inayotekelezwa mwa malengo ya amani na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani vitisho hivyo.
-
Vitisho vipya vya Trump dhidi ya Iran; ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na mkataba wa Umoja wa Mataifa
Dec 31, 2025 08:58Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu amesema kuwa, vitisho vya Trump dhidi ya Iran ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
-
Bunge la Iran lapongeza kurushwa kwa mafanikio satelaiti tatu katika anga za mbali
Dec 31, 2025 08:56Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imepongeza kurushwa kwa satelaiti tatu zilizotengenezwa zilizotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini, na kuitaja hatua hiyo kuwa mafanikio ya kihistoria katika mpango wa anga za mbali wa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Rais Pezeshkian: Iran itatoa jibu kali na la kumjutisha adui
Dec 31, 2025 07:59Rais wa Iran amesisitiza kwamba, jibu la Jamhuri ya Kiislamu kwa uchokozi wowote litakuwa kali na litamfanya adui ajute.
-
Araghchi aziandikia barua nchi jirani: Tutatoa jibu kali mno kwa uchokozi wowote dhidi ya Iran
Dec 31, 2025 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewaandikia barua mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa nchi jirani na kutaka kulaaniwa waziwazi na kwa uthabiti; bwabwaja na upayukaji wa Trump na Netanyahu akitangaza kwamba, Iran haitosita kutoa jibu kali na la kumjutisha yeyote atakayeshiriki kwenye uchokozi dhidi yake.
-
Dey 9, nembo ya mshikamano wa kitaifa mbele ya njama za maadui wa Iran
Dec 31, 2025 02:46Jana Jumanne, kona zote za Iran ya Kiislamu zilishuhudia maandamano makubwa ya wananchi ya kuadhimisha siku inayojulikana kwa jina la Dey 9 ambapo tarehe kama hiyo mwaka 1388 Hijria Shamsia (Disemba 30, 2009) mamilioni ya wananchi wa Iran walimiminika mitaani kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusambaratisha fitna kubwa ya adui.
-
Iran yajibu mapigo, yalitambua jeshi la majini la Canada kama shirika la kigaidi
Dec 30, 2025 23:29Iran imetangaza kulitambua Jeshi la Wanamaji la Canada kama shirika la kigaidi, ikijibu uamuzi wa huko nyuma wa Ottawa wa kuliorodhesha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kama kundi la kigaidi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema hayo jana Jumanne.
-
Velayati: Maadui walikosea sana kutweza nguvu za kijeshi za Iran
Dec 30, 2025 23:00Katibu Mkuu wa Majlisi ya Uamsho ya Kiislamu Duniani amesema kuwa, maadui wa Iran walikosea sana katika mahesabu yao juu ya nguvu za kijeshi za Jamhuri ya Kiislamu, kwani makombora yenye usahihi mkubwa ya Iran yalipenya safu nyingi za mifumo ya ulinzi na kupiga kwa usahihi shabaha zilizokusudiwa, na kubadilisha kikamilifu mlingano wa nguvu katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Majeshi ya Iran: Tumejiandaa kutoa pigo kali kwa uchokozi wowote wa adui
Dec 30, 2025 07:15Vikosi vya Ulinzi vya Iran vimetangaza kuwa, vimejiandaa kikamilifu kutoa majibu makali kwa tishio lolote la usalama wa Jamhuri ya Kiislamu na watu wake na kuonya kwamba, uchokozi wowote mpya wa uadui dhidi ya Iran utakuwa mkali zaidi, angamizi zaidi na wenye madhara makubwa zaidi kuliko huko nyuma.
-
Iran yaonya: Israel inalenga kudhoofisha uthabiti kwa kutambua 'Somaliland' kama nchi huru
Dec 30, 2025 03:07Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga kwa mara nyingine hatua ya utawala wa Kizayuni kutangaza kutambua eneo la Somaliland la Somalia kama nchi huru, ikieleza kuwa sehemu ya mkakati mpana wa kuleta machafuko katika eneo.