-
Mej. Jen. Baqeri: Ustawi wa Iran umeyaingiza kiwewe madola makubwa
Feb 09, 2021 07:30Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema leo kwamba madola makubwa duniani yameingiwa na kiwewe na wahaka kutokana na uwezo, ustawi na pia nafasi ya kistratijia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Ayatullah Raisi: Mauaji ya shahidi Suleimani na shahidi al Muhandis hayataachwa bila ya jibu
Feb 09, 2021 04:06Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, jinai iliyofanywa na Marekani ya mauaji ya makamanda wa muqawama haitaachwa bila ya jibu na akabainisha kuwa, shahidi Qassem Suleimani na shahidi Abu Mahdi al Muhandis ni mashujaa wa mapambano dhidi ya ugaidi.
-
Brigedia Jenerali Hatami: Sauti ya Israel ya kuitisha Iran ni kubwa, lakini haina ubavu wa kufanya lolote
Feb 08, 2021 22:59Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, sauti ya utawala haramu wa Israel ya kuitisha Iran ni kubwa, lakini kivitendo utawala huo hauna ubavu wa kufanya lolote dhidi ya taifa hili.
-
Salehi: Biden apate funzo kutokana na kushindwa mashinikizo na vitisho vyao vya miaka 42
Feb 08, 2021 12:09Mkuu wa Taasisi ya Atomiki ya Iran amesema kuwa, rais wa Marekani, Joe Biden, anapaswa awe amepata funzo kutokana na kushindwa vikwazo na vitisho vya miaka 42 vya serikali zilizopita za Marekani dhidi ya Iran. Amesema, hakuna ubaya wowote ambao mwanadamu anaweza kuufikiria ila serikali za Marekani zimeufanya dhidi ya taifa la Kiislamu la Iran lakini zimeshindwa.
-
Iran na Umoja wa Mataifa zajadili mgogoro wa Yemen mjini Tehran
Feb 08, 2021 08:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inaunga mkono kikamilifu jitihada za Umoja wa Mataifa za kujaribu kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Yemen.
-
IRGC yazionya nchi za eneo zinazofanya urafiki na Israel
Feb 08, 2021 08:47Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran (IRGC) ameonya kuwa, uwepo wa utawala wa Kizayuni katika eneo la Asia Magharibi hautaliletea eneo hili kitu kingine ghairi ya 'moto.'
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu: Wamarekani na Ulaya hawana haki ya kuweka masharti kwa Iran
Feb 08, 2021 05:21Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa Marekani na madola ya Ulaya hawana haki ya kuweka sharti lolote lile, kwani wao ndio waliokiuka makubaliano ya nyuklia; bali Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndio inayopaswa kuweka masharti kwa sababu imeheshimu na kufungamana kikamilifu na makubaliano hayo.
-
Kikosi cha Majini cha IRGC chapokea boti 340 za kivita zenye uwezo wa kurusha makombora + Video
Feb 08, 2021 04:41Kikosi cha Majini cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran (IRGC) kimepokea boti 340 za kivita zenye uwezo wa kuvurumisha makombora.
-
Mjumbe Maalumu wa UN nchini Yemen afanya mazungumzo na mshauri wa Zarif
Feb 08, 2021 04:33Mjumbe Malumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen amefanya mazungumzo na mshauri maalumu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambapo wamejadili matukio ya hivi karibuni ya Yemen.
-
Zarif: Iran haitajadili tena makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Feb 07, 2021 23:42Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yalijadiliwa na kukamilika na hayawezi kuzungumziwa tena.