-
Rais Rouhani: Serikali mpya ya Marekani ifidie makosa yaliyopita
Dec 09, 2020 08:50Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kuhusu udharura wa pande zingine zilizoafiki mapatano ya nyuklia ya JCPOA kufungamana na mapatano hayo na kusema: "Serikali mpya ya Marekani inapaswa kufidia makosa yaliyopita na kutekeleza kikamilifu ahadi zake kuhusu JCPOA."
-
Ayatullah Muhammad Yazdi wa Iran ameaga dunia
Dec 09, 2020 08:45Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Iran, Ayatullah Muhammad Yazdi, ameaga dunia leo na kurejea kwa Mola wake.
-
Feisal Miqdad: Uhusiano wa Iran na Syria ni mkubwa na wa kistratejia
Dec 09, 2020 03:56Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Damascus ni mkubwa na wa kistratejia na kueleza kuwa: Syria ina uhusiano mkubwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
-
Meja Jenerali Salami: Maadui wangojee jibu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Dec 08, 2020 23:59Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema: Maadui wangojee huku wakijua lazima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua kujibu kitendo cha kigaidi cha kumuua mwanasayansi wake bingwa wa masuala ya nyuklia na ulinzi.
-
Je, jukumu la Wakala wa Kimataifa wa Nyuklia IAEA ni kusimamia masuala kiufundi au kuvujisha ripoti za siri?
Dec 08, 2020 23:04Kushinikizwa kisiasa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA ni ushahidi kwamba umekuwa ukivujisha taarifa na ripoti za siri za wanachama wake, ni jambo ambalo limeibua maswali mengi yasiyo na majibu.
-
Rouhani: Iran itaendelea kuwa pamoja na serikali na taifa la Syria hadi ushindi wa mwisho
Dec 08, 2020 08:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesemam kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendeleza maamuzi na irada ambayo imekuwa ikichukua katika kuiunga mkono serikali na taifa la Syria kama nchi muitifakii wake wa kistratejia na itakuwa bega kwa bega na Syria hadi kupatikana ushindi wa mwisho.
-
Shamkhani: Wanaoanzisha uhusiano na Israel wasidhani watakuwa na mwisho mwema kuliko Gaddafi na al-Bashir
Dec 08, 2020 04:04Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, viongozi ambao kwa udhalili kabisa wanajishughulisha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kusaidia kutekeleza mipango michafu ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi wasidhani kwamba, watakuwa na hatima njema kuliko Kanali Muammar Gaddafi aliyekuwa kiongozi wa Libya au Omar Hassan al-Bashir, rais wa zamani wa Sudan
-
Jalali: Iran ina haki ya kulipiza kisasi kiistratijia; mauaji ya kigaidi ya shahid Fakhrizadeh
Dec 08, 2020 03:56Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Russia amesema kuwa, Tehran ina haki ya kulipiza kisasi mauaji ya kigaidi aliyofanyiwa mtaalamu wake wa nyuklia na masuala ya ulinzi, shahid Mohsen Fakhrizadeh.
-
Zulnouri: Wakala wa IAEA unampatia adui taarifa za Iran
Dec 08, 2020 02:46Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje Katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislam ya Iran (Bunge) amesema kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) unampatia adui taarifa za Iran na wala haulindi amana katika marhala mbalimbali.
-
Qalibaf: Mataifa ya Kiislamu yawatangazie walimwengu kwamba, kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni jambo baya
Dec 08, 2020 01:24Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, tawala na jamii za Kiislamu ziutangazie ulimwengu kwamba, kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel ni kitendo kibaya na kisichofaa.