Ayatullah Muhammad Yazdi wa Iran ameaga dunia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65097-ayatullah_muhammad_yazdi_wa_iran_ameaga_dunia
Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Iran, Ayatullah Muhammad Yazdi, ameaga dunia leo na kurejea kwa Mola wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 09, 2020 08:45 UTC
  • Ayatullah Muhammad Yazdi wa Iran ameaga dunia

Mwanazuoni maarufu wa Kiislamu nchini Iran, Ayatullah Muhammad Yazdi, ameaga dunia leo na kurejea kwa Mola wake.

Kwa mujibu wa taarifa, Ayatullah Mohammad Yazdi ambaye alikuwa amelazwa hospitalini, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 89. 

Hadi wakati wa kifo chake, Ayatullah Mohammad Yazdi, alikuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasomi na Wahadhiri wa Chuo cha Kidini cha Qum na pia mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.

Mwanazuoni  huyo, ambaye alitumia umri wake uliojaa baraka katika jihadi kwa njia ya Uislamu, aliwahi kuwa mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran kwa muda wa miaka 10. Aidha aliwahi pia kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu kati ya nyadhifa zingine muhimu.

Ayatullah Mohammad Yazdi wakati akiwa mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu

Mwanazuoni huyu mwanajihadi ameandika vitabu kadhaa na makala nyingi katika nyuga mbali mbali za Kiislamu.

Ayatullah Muhammad Yazdi atakumbukwa kwa ushujaa wake pamoja na ujasiri wake katika kutetea malengo matukufu ya Mapinduzi ya Kiislamu.