Rais Rouhani: Serikali mpya ya Marekani ifidie makosa yaliyopita
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65098-rais_rouhani_serikali_mpya_ya_marekani_ifidie_makosa_yaliyopita
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kuhusu udharura wa pande zingine zilizoafiki mapatano ya nyuklia ya JCPOA kufungamana na mapatano hayo na kusema: "Serikali mpya ya Marekani inapaswa kufidia makosa yaliyopita na kutekeleza kikamilifu ahadi zake kuhusu JCPOA."
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 09, 2020 12:20 UTC
  • Rais Rouhani: Serikali mpya ya Marekani ifidie makosa yaliyopita

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kuhusu udharura wa pande zingine zilizoafiki mapatano ya nyuklia ya JCPOA kufungamana na mapatano hayo na kusema: "Serikali mpya ya Marekani inapaswa kufidia makosa yaliyopita na kutekeleza kikamilifu ahadi zake kuhusu JCPOA."

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema  hayo leo Jumatano mjini Tehran katika kikao cha kila wiki cha baraza la mawaziri. Rais wa Iran amekumbusha kuwa nchi za Ulaya hazijafungamani na mapatano ya JCPOA na kuongeza kuwa, hatua ya Iran ya kuweka mashinepewa mpya katika kituo cha nyuklia cha Natanz imefanyika kwa mujibu wa tangazo la huko nyuma la Iran kupunguza uwajibikaji wake katika mapatano ya JCPOA, baada ya upande wa pili kukiuka mapatano hayo, na hivyo hilo si jambo jipya.

Rais wa Iran ameashiria pia matatizo ya Wizara ya Afya na Benki Kuu ya Iran katika kuzalisha na kununua chanjo ya corona na kusema: "Hili kundi ambalo lilikuwa katika Ikulu ya White House, na ambalo sasa liko katika siku zake za mwisho, lilikuwa khabithi kiasi kwamba limedhuru afya ya watu wa Iran." Amesema kundi hilo limekuwa na muamala fisadi na wa kinyama zaidi dhidi ya watu wa nchi za eneo na taifa adhimu la Iran."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema serikali yake iko tayari kuuza zaidi ya mapipa milioni mbili na laki tatu ya mafuta ghafi ya petroli mwaka ujao wa 1400 Hijria Shamsia (kuanzia Machi 21 2021). Aidha amesisitiza kuwa, bajeti ya Iran mwaka ujao haitategemea pato la mauzo ya mafuta kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Rais Rouhani pia amesea bajeti ya mwaka ujao umelipa kipaumbele maalumu suala ya kukidhi mahitaji ya kimaisha ya wananchi na kuwapunguzia mashinikizo.