Feisal Miqdad: Uhusiano wa Iran na Syria ni mkubwa na wa kistratejia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65089-feisal_miqdad_uhusiano_wa_iran_na_syria_ni_mkubwa_na_wa_kistratejia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Damascus ni mkubwa na wa kistratejia na kueleza kuwa: Syria ina uhusiano mkubwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 09, 2020 03:56 UTC
  • Feisal Miqdad: Uhusiano wa Iran na Syria ni mkubwa na wa kistratejia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa uhusiano wa Tehran na Damascus ni mkubwa na wa kistratejia na kueleza kuwa: Syria ina uhusiano mkubwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Aidha Feisal Miqdad ambaye yupo ziarani hapa nchini Iran amelaani kuuliwa kigaidi shahid Mohsen Fakhrizadeh mwanasayansi wa nyuklia na wa masuala ya ulinzi wa Iran na kueleza kuwa, serikali na wananchi wa Syria wako pamoja na taifa la Iran katika hali ngumu; na wana imani kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kufidia hasara hiyo kubwa na kuendeleza kasi yake ya mafanikio ya kielimu. 

Feisal Miqdad amesisitiza pia katika kukaribia kutimia mwaka mmoja tangu kuuliwa kigaidi Kamanda Luteni Jenerali Qassem Suleimani Mkuu wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) kwamba: shahid huyo mkubwa alikuwa na nafasi muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi wa Kizayuni na Marekani;  na kufelisha njama za Wazayuni na Marekani katika eneo hili. 

Shahid Qassem Suleimani 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, Wazayuni  wanayashambulia baadhi ya maeneo ya Syria kwa lengo la kuyasadia makundi ya kigaidi na kwamba: magaidi wamepata kipigo katika vita dhidi ya Syria, na ndio maana Israel inawashambulia makamanda wa Syria ili kufidia kushindwa kwake huko, kuigawa  na kuidhoofisha Syria.