-
Safari ya Waziri wa Nje wa Syria mjini Tehran; sisitizo la kudumishwa uhusiano wa kistratijia
Dec 07, 2020 23:34Akiwa katika safari yake ya kwanza kabisa nje ya nchi tokea ateuliwe kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Faisal al-Miqdad amefika mjini Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo na waziri mwenzake wa Iran, Muhammad Jawad Zarif na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Khatibzadeh: Misimamo ya Iran kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA haitabadilika
Dec 07, 2020 08:58Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa,misimamo ya Tehran kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA haitabadilika.
-
Vifaa vya satalaiti vilitumika katika mauaji ya kigaidi ya Shahidi Fakhrizadeh
Dec 06, 2020 21:56Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mauaji ya Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi bingwa wa Iran yalifanyika kwa kutumia vifaa vya kisasa vya kieletroniki vilivyokuwa vikiongozwa kwa satalaiti. Ameongeza kuwa, Wazayuni wanafahamu vyema kuwa jinai yao hiyo haitabaki bila kujibiwa.
-
Raisi: Uistikbari wa Marekani unajumuisha Wademocrat na Warepublican
Dec 06, 2020 21:54Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uistikbari na ubeberu wa Marekani unajumuisha vyama vyote viwili vikuu nchini humo vya Democratic na Republican na kuongeza kuwa, ni Iran yenye nguvu tu inayoweza kukabiliana na uistikbari.
-
Upayukaji wa viongozi wa Saudia dhidi ya Iran, ndoto za kufilisika kisiasa
Dec 06, 2020 21:44Viongozi wa Saudi Arabia ambao siku hizi nyoyo zao zimejaa hofu na woga kutokana na mabadiliko ya kisiasa ya eneo hili na matokeo ya kubwagwa Donald Trump huko Marekani, inaonekana wameshindwa kupata njia nyingine ya kujivua na lawama za kuchochea machafuko na ugaidi katika ukanda huu kwa kutumia fedha na fikra zao za ukufurishaji, ghairi ya kupayuka na kutuhumu watu wengine kwa mambo yasiyo na msingi.
-
Rais Rouhani: Trump anaondoka na ndoto zake za kufikisha mauzo ya mafuta ya Iran kiwango cha sifuri
Dec 06, 2020 08:24Rais Hassan Rouhani ameashiria vizingiti mbalimbali vya vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya mauzo ya mafuta na bidhaa za petrokemikali za Iran na kusema kuwa, Rais Donald Trump ameshindwa kutekeleza tumaini lake la kutaka mauzo ya mafuta ya Iran yafikie kiwango cha sifuri na sasa ataondoka madarakani pamoja na tarajio lake hilo.
-
Vifo vya Covid-19 vyaendelea kupungua nchini Iran
Dec 06, 2020 08:22Vifo vinavyotokana na Covid-19 vimeendelea kupungua katika siku za karibuni hapa nchini Iran ikiwa ni mafanikio ya kanuni na sheria mbalimbali zilizowekwa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona.
-
Kimya cha jumuiya na mashirika ya kimataifa; mhamasishaji wa ugaidi wa kiserikali
Dec 06, 2020 06:51Mauaji ya kigaidi aliyofanyiwa shahid Mohsen Fakhrizadeh, mwanasayansi bingwa wa masuala ya nyuklia na ulinzi ambaye pia alikuwa Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran yamelaaniwa na nchi nyingi duniani.
-
Gharib Abadi: Tutafuatilia kisheria kufichuliwa ripoti ya siri ya IAEA
Dec 06, 2020 03:53Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mashirika ya kimataifa yenye makao yao Vienna amesema, kuhusu kutangazwa katika chombo kimoja cha habari cha Magharibi ripoti ya siri ya hivi karibuni ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, kwamba karibuni hivi Iran italifuatilia kisheria na kwa uzito mkubwa suala hilo.
-
Kamanda Qaani: Kikosi cha Quds kiko mstari wa mbele kustawisha utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu
Dec 05, 2020 09:46Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema, kikosi hicho kinalinda na kiko mstari wa mbele katika kustawisha utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Ulimwengu wa Kiislamu.