-
Barua ya Zarif kwa Rais wa UNSC: Marekani haina haki yoyote ya kujaribu kurejesha vikwazo dhidi ya Iran
Aug 20, 2020 22:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akipinga hatua haramu na ya ukiukaji sheria ya Marekani ya kutaka kuzitumia vibaya taratibu zilizowekwa kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA za kurejesha upya vikwazo ilivyokuwa imewekewa Iran na akasisitiza kuwa Washington haina haki yoyote ya kujaribu kurejesha vikwazo hivyo.
-
Jeshi la Iran: Uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ni nembo ya kushindwa siasa za maadui
Aug 20, 2020 19:39Katika kuadhimisha Siku ya Sekta ya Ulinzi ya Iran tarehe 31 mwezi Mordad inayosadifiana na Ijumaa ya leo tarehe 21 Agosti, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa taarifa likisisitiza kuwa: Uwezo wa kiulinzi wa Iran umekuwa nemboya kushindwa siasa za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na jitihada za wataalamu na wanamapinduzi hapa nchini.
-
Uwezo mkubwa wa Iran katika uzalishaji wa silaha za kistratijia
Aug 20, 2020 19:36Iran kuwekewa vikwazo vya silaha kwa muda mrefu huenda kukawafanya baadhi ya watu kudhani kwamba baada ya kuondolewa vikwazo hivyo Iran ilipasa kubadilika na kuwa soko kubwa la mauzo ya silaha kwa maslahi ya nchi zinazozalisha silaha duniani ama ukweli wa mambo ni kinyume kabisa na dhana hii.
-
Zaidi ya wagonjwa 304,000 wa Covid-19 nchini Iran wamepata afueni
Aug 20, 2020 07:07Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, wagonjwa wengine wapya zaidi ya elfu mbili wa maradhi ya Covid-19 wamegunduliwa nchini, huku idadi ya waliopata afueni ya ugonjwa huo ikipindukia 304,000.
-
Iran yazindua injini ya mvuke ya ndege ya kizazi cha nne na aina mbili mpya za makombora
Aug 20, 2020 03:40Injini ya kwanza ya mvuke ya ndege ya kizazi cha nne pamoja na aina mbili za makombora ya balestiki na kruzi yamezinduliwa hapa nchini katika hafla iliyofanyika leo na kuhudhuriwa na Rais na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
-
Rais Rouhani: Jitihada mpya za Marekani dhidi ya Iran zitafeli
Aug 19, 2020 05:45Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jitihada mpya za Marekani za kutumia azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kutoa pigo kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA tayari zimeshafeli.
-
Wanafunzi nusu milioni raia wa kigeni wanasoma Iran bila malipo
Aug 19, 2020 03:11Waziri wa Elimu Nchini Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa elimu bila malipo yoyote kwa zaidi ya wanafunzi nusu milioni wa kigeni.
-
Iran haina tatizo katika kuzalisha silaha za kistratijia
Aug 18, 2020 21:58Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Iran haina tatizo katika uzalishaji wa silaha za kistratijia.
-
Ayatullah Khamenei: Taskhiri ametoa huduma kubwa kwa Ulimwengu wa Kiislamu
Aug 18, 2020 09:59Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kwa mnasaba wa kuaga dunia mwanazuoni, mujahid na mtetezi wa Uislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Muhammad Ali Taskhiri aliyekuwa kiongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu ya Kiislamu na Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Ulimwengu wa Kiislamu.
-
Tuhuma za Marekani dhidi ya Iran; kuwabebesha lawama wasiohusika ili kutetea uingiliaji katika masuala ya eneo
Aug 18, 2020 03:37Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema, matukio yanayojiri leo hii huko Afghanistan ni matunda ya uingiliaji na uwashaji moto wa vita uliofanywa na Marekani ndani ya nchi hiyo.