Jeshi la Iran: Uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ni nembo ya kushindwa siasa za maadui
(last modified Fri, 21 Aug 2020 00:09:20 GMT )
Aug 21, 2020 00:09 UTC
  • Jeshi la Iran: Uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ni nembo ya kushindwa siasa za maadui

Katika kuadhimisha Siku ya Sekta ya Ulinzi ya Iran tarehe 31 mwezi Mordad inayosadifiana na Ijumaa ya leo tarehe 21 Agosti, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa taarifa likisisitiza kuwa: Uwezo wa kiulinzi wa Iran umekuwa nemboya kushindwa siasa za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na jitihada za wataalamu na wanamapinduzi hapa nchini.

Taarifa ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa: Katika miaka ya karibuni sekta ya ulinzi ya nchi hii imepiga hatua kubwa na zenye taathira kwa ajili ya kuiondoa sekta ya binafsi ya Iran katika minyororo ya vikwazo vya kidhulma vya ubeberu wa kimataifa. 

Taarifa ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imeashiria kushindwa kwa fedheha Marekani kuongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa: Katika miongo kadhaa iliyopita Marekani imetekeleza njama za aina mbalimbali za kuiarifisha Iran kuwa tishio sambamba na kuziuzia  silaha nchi za kanda hii na hivyo kulifanya eneo la Asia Magharibi kuwa ghala kubwa la zana za kijeshi; lakini nchi hiyo siku zote imekuwa na inaendelea kuhofia uwezo wa ndani na wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limesisitiza kuwa: Jeshi litaendelea kuwa bega kwa bega na sekta ya kuzalisha zana za ulinzi katika njia ya jihadi ya sayansi na utafiti na katika kupata teknolojia ya kisasa ya ulinzi na silaha za kistratejia katika nyuga mbalimbali za nchi kavu, anga, baharini na katika sekta ya kutengeneza makombora ili nchi iweze kufuata njia mwafaka haraka iwezekanavyo.  

Wakati huo huo, maonyesho ya mafanikio ya uwezo wa ndege zisizo na rubani (droni)  za Iran na uundaji wa injini ya Owj yalifunguliwa jana kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuzinduliwa kombora la balestiki lililopewa jina la Shahidi Haj Qassem Soleimani lenye uwezo wa kupiga umbali wa kilomita 1400 na pia kombora la Cruise lililopewa jina la Shahidi Abu Mahdi lenye uwezo wa kulenga shabaha umbali wa kilomita 1000 pamoja na injini nyepesi ya Turbofan kama mafanikio ya taifa ya Wizara ya Ulinzi ya Iran. 

Rais Rouhani na Waziri wa Ulinzi, Brigedia Jenerali Amir Hatami  

 

Tags